Bunge wa viti maalum mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) DR Ritta Kabati akiwa kwenye moja ya majukumu yake ya kuwatumikia watanzania kama ambavyo Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka wabunge wote kuwatumikia wananchi (PICHA KUTOKA MAKTABA)
Bunge wa viti maalum mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) DR Ritta Kabati akitoa msaada wa vifaa vya walemavu wa viongo lengo likiwa ni kuunga mkono Bunge wa viti maalum mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) DR Ritta Kabati. (PICHA KUTOKA MAKTABA)Na Fredy Mgunda,Iringa.

 

BUNGE wa viti maalum mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) DR Ritta Kabati amesema kuwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewaheshimisha wanawake kwa utendaji wake wa kazi katika kuliongoza Taifa la Tanzania.

 

Akizungumza na blog hii mbunge huyo DR Kabati alisema kuwa toka ameteuliwa kuwa Rais wa Tanzania amefanya kazi kubwa ya kuleta maendeleo na kuonyesha kuwa yeye ni kiongozi bora ambaye anaweka kulifikisha taifa hili katika nchi ya ahadi.

 

Dr Kabati alisema kuwa Rais Samia toka ameingia madarakani amefanikiwa kuwaamini wanawake katika utendaji wa nyazifa za ngazi ya juu na wanawake hao wamekuwa wanafanya kazi hizo vizuri tofauti na ilivyokuwa kwenye fikra za watanzania wengi.

 

“Lakini Mheshimiwa Rais mwanamke huyu ametupa upendeleo na ametuamini sana wanawake wenzie na ametoa nafasi nyingi za upendeleo kwa wanawake ambao wanauwezo wa kuongoza nafasi hizo na wanamsaidia kweli kweli” alisema Dr Kabati

 

Alisema kuwa kuna mawazi wengi wanawake ambao wamekuwa wanafanya kazi kubwa ya kuleta maendeleo kwenye wizara zao kama vile waziri wa ulinzi,waziri wa afya,waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum na manaibu mawaziri wengi kwenye wizara mbali mbali na wanafanya kazi vizuri.

 

DR Kabati alisema kuwa kuna wakuu wa wilaya,wakuu wa mikoa, maneja  na wakurugenzi wanawake wengi na wamekuwa wanafanya kazi nzuri ya kumsaidia Mheshimiwa Rais kuleta maendeleo kwa watanzania.

 

Alisema kuwa katika maeneo ambayo wanawake wamepewa nafasi ya kuongoza kumekuwa na mabadiliko ya haraka ya kimaendeleona yanaonekana kutokana na wanawake wengi wamezaliwa kuwa viongozi toka wakiwa kwenye ngazi ya familia.

 

Dr kabati alisema kuwa watanzania wanatakiwa kuendelea kumuamini na kumuunga mkono Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuleta maendeleo kwa wananchi wa Tanzania.

 

Alisema kuwa kwa kipindi cha mwaka mmoja wa madaraka yake amefanikisha miradi mingi na mikubwa ya kimaendeleo kwa wananchi na kuwapunguzia adha ya kuchangia maendeleo kwa kiasi kikubwa.

 

Dr Kabati alimazia kwa kusema kuwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa mwaka mmoja tu amefanya mabadiliko makubwa ya kimaendeleo kwa wananchi wa Tanzania na atakiwa kuendelea kupewa heshima anayostahili.

 

Alisema kuwa Rais Samia ameondoa mateso ya Bodi ya Mikopo uliowatesa wafanyakazi kwa miaka kadhaa kwa kuondoa tozo ya kutunza thamani ya mkopo  ambayo ilikuwa inaongeza mkopo kila mwaka badala ya kupunguza.

Dr Kabati alisema kiburi cha madaraka kwa wakuu na watendaji wa taasisi kimepungua, kuongezeka kwa amani na utulivu ofisini mwa wafanyakazi kutokana na mabadiliko hayo.

“Awali, wafanyakazi wengi walikuwa katika hali ya uoga na njia panda kutokana na vitisho, pia kufufuka kwa matumaini ya maboresho ya mishahara iliyosimamishwa kupandishwa kwa miaka mitano iliyotangulia, hii ni baada ya kutoa ahadi ya kuboresha maslahi ya mishahara katika sherehe za Mei Mosi jijini Mwanza mwaka 2021,”amesema.

Dr kabati amesema kuendelea kulipwa malimbikizo ya mishahara na maslahi mengine kwa awamu mbalimbali na kuongeza kwa umri wa wanufaika wa Bima ya Afya kutoka miaka 18 hadi 21

 

Na ikumbukwe kuwa Mwishoni mwa juma hili itakuwa ni mwaka mmoja tangu Samia Suluhu Hassan ambae alikuwa Makamu wa rais wa Tanzania aliposhika hatamu za nchi hiyo kufuatia kifo cha mtangulizi wake hivyo kuwa mwanamke wa kwanza kuongoza taifa hilo.

 

 

Aliapishwa, katikati ya kipindi cha janga la corona, mwezi Machi baada ya mtangulizi wake John Magufuli alipofariki ghafla alipokuwa madarakani. Na mara tu aliposhika uongozi, alinukuliwa akisema kuwa ‘‘yeye na Magufuli walikuwa kitu kimoja.’’

 

Share To:

Post A Comment: