Na Ahmed Mahmoud 

 Kamati ya siasa mkoa wa Arusha imekabidhiwa Miradi ya madarasa 105 iliyogharimu takribani bilion 2.1 zikiwa ni fedha za Uviko 19 zilitolewa na serikali kwa jiji la Arusha ikiwa ni Utekelezaji wa Ilani ya CCM. 

 Akitoa taarifa ya Utekelezaji miradi hiyo wakati wa ziara ya kamati ya siasa ya CCM mkoa wa Arusha,Mkuu wa Wilaya ya Arusha Said Mtanda amesema miradi hiyo serikali imekabidhi ili kamati hiyo wakabidhi kwa wananchi.

Amesema kuwa pamoja na kukamilika kwa madarasa hayo ambayo yatachagiza ufaulu tunamshukuru Sana mkuu wa mkoa wa Arusha kwa kuyasimamia kwani wakati Mimi nakuja hapa nimekuta yapo asilimia 90. 


 Amesema serikali ya awamu ya sita imehakikisha inaondoa changamoto za madarasa sanjari na kuongeza ufaulu kwa wanafunzi ndio maana Wilaya hii inaongoza kitaifa kwa sababu tumekuwa tukitoa chakula kwa wanafunzi mashuleni. 

"Tumejipanga kisawa sawa na wadau wa elimu tumetenga milion 80 kuhakikisha ufaulu unaongezeka na mwisho wa mwezi huu tutandaa hafla ya kuwapongeza waalimu ikiwa kama motisha ya kutambua mchango wao katika kukuza elimu" Awali akiongea Mara baada ya makabidhiano hayo Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM taifa Denilson Palangyo ametoa agizo kwa madiwani kuisemea miradi kwa wananchi. 

 Amesema kuwa ipo haja kwa kamati za siasa za kata kufanya ziara za kutembelea miradi ya elimu kwa lengo la kwenda kuielezea kwa wananchi hili ni agizo la kamati ya siasa kwa madiwani wanaotokana na chama hichi.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Joseph Massawe akiopokea miradi hiyo ameipongeza serikali kwa hatua nzuri ya kukamilisha madarasa hayo hatua iliyosaidia kuondoa changamoto za msongamano madarasani.

Nae Mkuu wa shule ya sekondari Arusha Lorina Ntelesi amesema kwamba mradi huo umekamilika na umeondoa changamoto ya uwepo awamu mbili za wanafunzi kuingia shuleni ila Sasa wanafunzi wote 600 wameingia Darasani.

Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: