Na Mwandishi wetu,Mbeya.TAASISI ya Tulia Trust imeitunuku Cheti Kampuni ya Magazeti ya Serikali ya,Tanzania Standard Newspapers(TSN) kama sehemu ya kutambua mchango wake  katika kufanikisha  Tamasha la ngoma za jadi za Tulia Traditional Dances Festival 2021 lililofanyika Septemba 23 hadi 25 mwaka jana jijini Mbeya.


 


Akikabidhi Cheti hicho katika ofisi za TSN za Kanda ya Nyanda za Juuu Kusini zilizopo Mtaa wa Accasia eneo la Uhindini Kata ya Sisimba jijini Mbeya,Meneja wa Tulia Trust,Jackline Boaz alisema Kampuni hiyo ilitoa ushirikiano mkubwa kwenye tamasha hilo tangu wakati wa maandalizi,lilipokuwa likifanyika na hata baada ya kumalizika kwake.


 


Jackline aliyapongeza Magzeti yanayozalishwa na TSN ya Habarileo na Dailynews akisema yaliwezesha kwa kiasi kikubwa matukio yaliyokuwa yakiendelea juu ya Tmasha hilo kufahamika katika maeneo mengi ndani na nje ya nchi kutokana na habari zilizokuwa zikichapishwa.


 


“Wakati wote tuliziona kazi zilizochapishwa na magazeti ya kampuni hii.Hakina wanahabari wa TSN hawakuwa nyuma..tulikwenda nao sambamba na kutudhirishia kuwa jambo hili ni kubwa na tulipokea simu kutoka maeneo mengi kwa watu waliokuwa wakuatilia tukio lile kupitia magazeti ya TSN na pia mitandao ya kijamii iliyopo chini ya kampuni hii pendwa.” Alisema Jackline.


 


Aliahidi Taasisi hiyo kuendelea kuwa na ushirikiano wa karibu na TSN huku akiuomba uongozi wa kampuni hiyo kuendelea kufanya kazi na wadau mbalimbali wanaoonesha nia ya kuwaina watanzania kupitia Nyanja mbalimbali.


 


Akipokea Cheti hicho kwa niaba ta TSN,mwandishi wa gazeti la Habarileo mkoani Mbeya,Joachim Nyambo alipongeza hatua ya Tulia Trust kutambua na kuupa thamani mchango wa vyombo vya habari vilivyo chini ya kampuni hiyo akisema hatua hiyo inaongeza ari ya kuendelea kufanya kazi kwa bidii.


 


Nyambo alisema wapo wadau wengi wanaohudumiwa na vyombo vya habari hususani vilivyopo chini ya serikali lakini ni wachache wanaoweza kutambua mchango wa vyombo hivyo na kuupa thamani hata wakarudi kuja kutoa mrejesho kama ilivyofanywa na Taasisi hiyo iliyo chini ya Mbunge wa Mbeya mjini na Spika wa Bunge,Dk Tulia Ackson.


 


Aidha alisema kwakuwa TSN ipo kwaajili ya kuwatumikia watanzania haitosita kushirikiana na mdau yeyote mwenye malengo ya kuwafanya wananchi wapige hatua kimaendeleo na badala yake itatoa ushirikiano wa kutosha kama ilivyofanya kwenye Tamasha hilo lenye lengo la kuibua na kukuza vipaji vya sanaa nchini.


 


“Sote ni mashahidi tangu kuanza kwa Tamasha hili la ngoma za jadi la Tulia kumekuwa na mwamko mkubwa wa kuibuliwa kwa ngoma za asili tofauti na ilivyokuwa awali.Watu sasa wanaziona ngoma za asili kama fursa.Sasa mdau anayeibua mambo kama haya sisi TSN hatuwezi kumwacha afanye peke yake..tutakuwa nae tu.” Alisisitiza Nyambo.


 

Share To:

Post A Comment: