Wanamuziki wakiwa katika picha ya pamoja jijini Arusha kwenye moja ya matukio yao. Umoja wa Wanamuziki hawa unaweza kuwa chachu ya kusaidiana katika masuala mbalimbali hata mmoja kati yao anapokuwa mgonjwa. 
Mchungaji Mary Nyerere ambaye aliongoza maombi hayo.
Katibu Mkuu wa TAMUFO Stellah Joel.
Mlezi wa TAMUFO Dk.Frank Richard. Na Dotto Mwaibale 


WANAMUZIKI wa Arusha kupitia Umoja wa Wanamuziki Tanzania  (TAMUFO) wameungana na Watanzania kumuombea Mwanamuziki wa bongo fleva Profesa J ambaye amelazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu.

Akizungumza na waandishi wa habari Katibu Mkuu wa TAMUFO Stellah Joel alisema maombi hayo yamefanyika leo katika Uwanja wa Makumbusho ya Elimu Viumbe Jijini Arusha.

Joel alisema waliamua kuandaa maombi hayo kwa kuzingatia kuwa Profesa J ni mwanamziki mkongwe wa muziki wa kizazi kipya na kupitia muziki ameweza kufundisha mengi kupitia burudani aliyokuwa akiitoa na pia kupitia Ubunge amelitumikia Taifa kwa namna moja au nyingine hivyo kila mmoja wetu anapaswa kumuombea katika kipindi hiki kigumu cha kuumwa kwake.

"Kipindi hiki anachokipitia mwenzetu licha ya Serikali kutamka kuwa itagharamia matibabu yake lakini sisi kama wadau wa muziki tuna kila sababu ya kuendelea kumsapoti mwenzetu kwa hali na mali" alisema Joel.

Mlezi wa TAMUFO Dk.Frank Richard ameishukuru Serikali kwa kuanza gharamia matibabu yake ni jambo la kizalendo.na upendo mkubwa.

"Serikali kwa nyakati tofauti imekuwa ikiwasaidia wanamuziki wanapo kuwa katika changamoto mbalimbali hasa ya kuumwa jambo ambalo linatia moyo" alisema Richard.

Pia amewashukuru watanzania wote walioanza kutoa michango yao kwa ajili ya kuongeza nguvu ya kumsaidia Profesa J.

 Aidha Dk.Richard ameendelea kuipongeza Serikali kwa kutoa Bima ya Afya NHIF kwa Wanamuziki kwa gharama nafuu kupitia Taasisi Ya TAMUFO ambayo imewawezesha kumudu gharama za vipimo na matibabu katika Hospital za Serikali na za Binafsi.

Mchungaji Mary Nyerere ambaye aliongoza maombi hayo amewashukuru watu wote waliochukua hatua ya kumwombea Profesa J na kueleza kuwa hakuna lisilowezekana kwa Mungu.

Pastor Nyerere alisema kuna nguvu katika maombi na maombi ya mwenye haki yanafaa hasa akiomba kwa bidii.

Alisema wataendelea kumuomba Mungu kwa bidii na kuwa utafanyika uponyaji kwa Profesa J na kurejea kwenye afya yake ya kawaida.

Share To:

dottomwaibale

Post A Comment: