************************

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa, amewataka wasanii na watengenezaji wa Tamthilia ya HUBA inayorushwa na DStv kuutangaza utamaduni wa Tanzania duniani ili wageni wengi watembelee nchi hiyo.

Mhe. Mchengerwa amesema hayo leo Februari 12, 2022 jijini Dar es Salaam wakati akiagana na kundi hilo lililoondoka kwenda nchini Dubai kuandaa kazi zao.

Amesema dhamira ya Serikali ni kuona filamu za Tanzania zinakuwa na ushindani katika soko la kimataifa.

Katika tukio hilo Mhe. Mchengerwa ameambatana na Katibu Mkuu wa wizara Dkt. Hassan Abbasi na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Dkt. Kiagho Kilonzo ambao wote walizawadiwa vyeti vya shukrani kwa kutambua mchango wao kwenye tasnia ya Filamu.
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: