Na Mwandishi Wetu.

 Leo Januari 24, 2022 Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye amefanya Ziara ya Kikazi katika kampuni ya Mawasiliano ya Tigo na kujionea kampuni inavyofanya kazi . Akizungumza baada ya Ziara iyo Waziri Nape ameyapongeza Makampuni ya Simu nchini kwa kuendelea kutoa huduma zinazochangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa sekta ya Mawasiliano nchini. 


"Makampuni ya Simu yamechangia pakubwa katika maendeleo ya nchi yetu maana wanalipa kodi, wanaajili Watanzania wengi sana hasa vijana , lakini pia huduma zao zinasaidia huduma nyingine mfano ulipaji wa kodi, utumaji na upokeaji wa fedha na mambo mengine kadha wa kadha kwahiyo mchango wao ni Mkubwa Sana" Alisema Waziri Nape.


Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo CPA Innocent Rwetabura amemshukuru Waziri Nape kwa kufanya Ziara hiyo 

" Sisi kama Tigo Tanzania ni Kampuni ambaye tumewekeza zaidi ya Dola Bilioni 1.5 toka tumeanza , na tunatarajia kuwekeza zaidi ya Milioni 500 kuanzia sasa hivi kwa miaka mitano ijayo ili kuweza kuboresha Mawasiliano  na ubora wa huduma Tunazotoa , kwa kipindi cha mwaka jana tumeweza kulipa kodi ambayo inafikia kiasi cha Shilingi Bilioni 370 , pamoja na kuajiri zaidi ya elfu moja mia mbili thelathini na tatu (1,233) na Mawakala zaidi ya laki mbili na elfu ishirini " Alisema Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo CPA Innocent Rwetabura



Share To:

Adery Masta

Post A Comment: