Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Innocent Bashungwa ameshiriki maziko ya  Mke wa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Martine Shigela yaliyofanyika wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.


Akitoa salamu za serikali, Mhe. Bashungwa ametoa pole kwa familia kwa msiba huo mzito.


Amesema kutokana na wema wa Mhe.Shigela ndio sababu ya watu wengi wamejitokeza kumfatiji kufuatia msiba huo wa mke wake.


"Mhe. Martine  ni mtu mwema mwenye ushirikiano wa hali ya juu tangu nilipokutana naye  nikiwa Wizara ya Viwanda na biashara, Kilimo na hadi leo hii,"amesema

 

Mhe. Bashungwa amesema @ortamisemi inatoa pole na kuwashukuru Wakuu wote wa Mikoa Tanzania bara kwa ushirikiano walionyesha katika kupindi hiki kigumu cha msiba wa Bi. Magdalena aliyefariki   tarehe 20.01.20211 na hadi anazikwa leo tarehe 24.01.20211 Wilayani humo.



Marehemu Magdalena Layda Shigela alikuwa Afisa Elimu vielelezo na Takwimu katika Jiji la Dar es salaam na alifunga ndoa na Mhe. Martin Shigela Machi,2017.

Share To:

Post A Comment: