Na Elizabeth Joseph,Mbeya.


BAADHI ya Watumishi wa huduma za Hoteli mkoani Mbeya wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan  kukubali Nchi ya Tanzania kupata chanjo ya kujikinga na mlipuko wa ugonjwa wa Homa ya Mapafu inayosababishwa na virusi vya UVIKO-19.


Waliyasema hayo kwa nyakati  tofauti wakati wakiongea na waandishi wa habari Wanawake kutoka mikoa mbalimbali nchini walipofanya ziara ya kutembelea vivutio vya Utalii na Uwekezaji mkoani Mbeya.


Walieleza kuwa uwepo wa chanjo nchini imesaidia kuondoa athari za zilizojitokeza kutokana na mlipuko wa ugonjwa huo ambapo sekta ya Utalii kwa ujumla ikiwemo hoteli na nyumba za kulala wageni ziliathirika kwa kukosa wageni.


Hotman Nyagawa ni Meneja Kampuni ya Usingilo ambao pia ni wamiliki wa Hoteli ya Usungilo iliyoko Kata ya Forest Mbeya mjini allibainisha kuwa ujio wa chanjo ya UVIKO 19 imewezesha sekta ya Utalii kuanza kurejea katika hali yake kawaida kama zamani kwakuwa biashara imeanza kuonekana kwa kupata wateja.


"Mwaka 2020/21 sekta ya Utalii ikiwemo hoteli na nyumba za kulala wageni tuliathirika kwa kiasi kikubwa,hali ilikuwa mbaya hatukuwa tukipokea wageni pia sisi kwa sisi tulikuwa tunaogopana, tunamshukuru sana Rais Samia kwa kuwezesha nchi kupata chanjo watu wamechanja na hivi sasa wanaendele na shughuli zao kama kawaida hata kwetu wa huduma za hoteli tumeanza kupokea wageni,"Aliongeza kusema.


Naye Meneja wa Hoteli ya Desderia Bw, William Jima aliwaomba Watanzania kuchanja chanjo ya UVIKO 19 ili kujikinga na mlipuko wa ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na kuendelea kufanya kazi za kujikwamua kiuchumi wakiwa na kinga hiyo.


"Nawashauri watu wakachanje ili maisha yaweze kuendelea kwani ukichanja unakuwa umejikinga na mlipuko wa COVID-19, tusipuuze kuchanja maana ni kawaida yetu japo kuchanja ni hiari basi tuhamasike,"Alisema Bw, Jima.


Hivi karibuni Rais, Samia amezindua Kampeni ya kuchanja kwa hiari zoezi linaloendelea kutolewa nchi nzima  katika vituo vya kutokea huduma za afya ambapo kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Afya hadi kufikia mwezi Oktoba mwaka huu watu waliochanjwa chanjo hiyo ni 760,962 kwa Tanzania Bara huku Zanzibar zikionesha watu 10,800 walipata chanjo hiyo.

Share To:

Post A Comment: