Na Angela Msimbira MVOMERO


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  Mhe. Ummy Mwalimu  amesema ataunda timu kutoka Ofisi ya Rais - TAMISEMI kuchunguza  matumizi ya shilingi milioni 700 zilizotakiwa kujenga bweni na bwalo katika shule ya Sekondari ya Sokoine Memorial katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro


Ameyasema hayo wakati akikagua ujenzi wa shule hiyo leo na kusema kuwa  hajaridhishwa na matumizi ya fedha zilizopokelewa kwa ajili ya ujenzi wa bweni na bwalo katika shule hiyo


"Sijaridhishwa na matumizi  ya fedha  shilingi milioni 700 zilizotolewa kwa ajili ya Ujenzi wa bweni na bwalo la shule hiyo, uhalisia hauonekani" amesisitiza Waziri Ummy


Waziri Ummy amesema kuwa wataalam hao watatakiwa kuangalia thamani ya majengo yaliyojengwa wakilinganisha na fedha zilizotumika ili kuweza kutoa ushauri  kiasi cha fedha kinachotakiwa kukamilisha  majengo hayo. 


Aidha amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuzingatia utaratibu wa matumizi ya fedha za Serikali.

Share To:

Post A Comment: