Na Lucas Myovela_ Arusha.


Wafanya biashara Jijini Arusha Philemon Mollel maarufu MONABANI na mwenzake Baraka Titus Mollel, Leo Septemba 9,2021. Wamefikishwa Katika Mahakama ya Wilaya ya Arusha mbele ya hakimu Salome Mshasha na kusomewa Mashtaka yao yanayo wakabili ya Matumizi mabaya ya Silaha kinyume cha kifungu cha sheria 84/35 cha kanuni ya adhabu kamailivyofanyiwa marekebisho mwaka 2019.

Wakisoma mashtaka hayo mbele ya Mahakama Mwanasheria wa Serikali Brandina Msawa alieleza kuwa mnamo tarehe 18.5.2021, Mtuhumiwa namba Moja Philemon Mollel alifika katika kituo cha mafuta cha Saiteru Petrol Station na kumkuta mshatikwa wa Pili Titus Mollel ndipo Philemon kuanza kufyatua risasi kwa muelekeo aliyokuwepo Titus na ndipo Titus nae akaanza kujibu kufyatua risasi kwa kumuelekezea Philemon.

Wapili kutoka kushoto ni Mshtakiwa namba moja katika shtaka hilo Ndg Philemon Mollel maarufu kama Monabani, wakwanza kushoto ni Wakili Msomi Mgalula.

Brandina anaendelea kueleza Mahakama baada ya tukio hilo lilizua taaruki kwa wananchi waliyokuwepo katika eneo hilo na ndipo polisi walipewa taarifa na waliweza kufika katika eneo hilo la tukio na kuwashikia washtakiwa wote wawili waliweza kukamatwa na kufikishwa katika kituo cha polisi na kufunguliwa Mashtaka na leo hii kufikoshwa mahakamani.

Mwanasheria wa Serikali alieleza mahakama kuwa baada watuhumiwa wote kukamatwa wali weza kupakuliwa nyumbani kwao na maungoni ambapo mshtakiwa wa kwanza Philemon Mollel alikutwa na bastola moja, Nyumbani kwake na Magazine mbili na risasi 25 pamoja na mkoba wa kutunzia silaha ambavyo vyote vimeshikiliwa.

Pichani ni Mfanyabiashara Titus Mollel

Aidha pia kwa Mshtakiwa wa pili Titus Mollel yeye alipekuliwa maungoni na kukutwa na bastola moja na kuchukuliwa vitabu vya umiliki wa silaa pamoja na leseni ya umiliki wa silaha hiyo na vyote vimeshikiliwa.

Kwa upande wa watuhumiwa wote walikana mashtaka hayo yanayo wakabili na kesi hiyo imehairishwa hadi tarehe 27.9.2021 ambapo itaendelea kusikizwa na kutolewa ushahidi kwa upande wa mashtaka ambapo imesema itakuwa na Mashahidi sita pamoja na vielelezo 16 katika kesi hiyo.

Kwa upande wa watuhumiwa wote wawili mtuhumiwa wa kwanza Philemon Mollen anatetewa na wakili Msomi Kapimpiti Mgalula, huku mtuhumiwa wa pili Titus anatetewa na wakili msomi David Makata na 
Watuhumiwa wote wawili kwa pamojaa wapo nje kwa dhamana.
Share To:

Lucas Myovela

Post A Comment: