Na Joachim Nyambo,Mbeya.

UKOSEFU wa taarifa za uhakika katika ngazi za vijiji na mitaa umetajwa kuwa sehemu ya changamozo zinazosababisha watoto walio katika umri mdogo katika kaya masikini kutopata wahisani wa kuwasaidia kuanza kujenga misingi bora ya maisha yao ya baadaye ikiwemo katika elimu.

Hayo yamebainishwa na wadau mbalimbali wa maendeleo mkoani Mbeya walipoizungumzia siku ya Hisani duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Septemba tano ya kila mwaka.

Wadau hao wamesema vipaji vya watoto wengi vimekosa misingi imara kutokana na familia zao kuwa na maisha duni huku wahisani wengi kutoka ndani na nje ya nchi wakionekana kujitokeza pale mtoto anapoonekana kushindwa kuendeleza kipaji chake akiwa amefikia katika umri mkubwa.

Miongoni mwa wadau waliozungumzia hali hiyo ni Mkurugenzi wa Shirika la wanahabari la Elimisha,Festo Sikagonamo aliyesema wapo watoto wadogo wengi wanaohitaji kusaidiwa hasa katika hatua za awali za malezi na makuzi ikiwemo kuanza elimu ya awali na msingi lakini hawajapata wahisani wa kuwasaidia.

Sikagonamo alisema wapo pia wahisani ambao wangependa kuwasaidia watoto walio katika umri mdogo kuanza kuimarisha misingi ya ndoto na vipaji vyao lakini hawana taarifa juu ya watotgot walio na uhitaji.

Alisema wahisani wengi wamebakia kuzipata taarifa kwa watoto wanaobahatika kufikia hatua zaidi ya ndani ya familia zao ikiwemo kwenye vituo vya kulelea watoto yatima au wale wanaofika kwenye taasisi na kutoa kilio chao juu ya kukwama na kushindwa kuendeleza kile wanachokipenda maishani mwao.

“Kuna changamoto kwa watoto wadogo ..taarifa za hawa watoto wadogo walio na uhitaji  upatikanaji wake wakati mwingine unakuwa ni mgumu..mara nyingi sana hata taarifa zinazopatikana kwa hawa watoto wadogo ili waweze kupata misaada  zinapatikana kwa wale ambao wapo kwenye vitu maalumu ambao wanaweza wakawa ni yatima..sasa wahisani wanakwenda kupata taarifa huko.” Alisema Sikagonamo

“Kuna watoto ambao wana uhitaji mkubwa sana na wanaishi kwenye familia ambazo ni masikini lakini taarifa zinawezaje kuwafikia wahisani ili waweze kujua katika kaya flani  kuna mtoto ambaye ana uhitaji wa msaada.

Mkurugenzi huyo alishauri Taarifa za Mpango wa kusaidia kaya masikini unaoratibiwa na Mfuko wa maendeleo ya jamii nchini (TASAF III) kuwezeshwa kuwa na wigo mpana zaidi  ili ziweze kuwaibua watoto walio na uhitaji wa kufika mbali zaidi  lakini hawajulikani  kwa wahisani


Alisisitiza pia Mfumo wa ufuatiliaji wa taarifa za vizazi na vifo kuanzia ngazi za mitaa na vijiji kutiliwa mkazo akisema kufanya hivyo kunawezesha jamii ya sehemu husika kuwatambua watoto walio na uhitaji wa kukutanishwa na wahisani tangu wangali wadogo kwakuwa taarifa za kaya husika zitabainisha mahitaji yaliyopo.


 


Mkurugenzi wa shule ya mchepuo wa kiingereza ya Hollyland Pre & Primary School,Lawena Nsonda ambaye amekuwa mmoja wa wahisani wa ndani kwa kuwasaidia baadhi ya watoto wanaotoka katika kaya zisizo na uwezo kuanza masomo kwenye shule yake alisema wapo watoto wengi walio na uhitaji lakini hawajakutanishwa na wahisani.


 


Nsonda maarifu kwa jina la Baba mzazi alisema ipo haja ya kuandaliwa kwa mfumo utakaowezesha watoto wadogo walio na uhitaji kukutana na wahisani ili wasaidiwe kutimiza ndoto zao kuanzia katika ngazi za awali hususani katika Nyanja za elimu na afya bora.


 


Mkuu wa shule ya Hollyland Pre & Primary School,Kenya Mahada alisema watoto wanaofadhiliwa na shule wanaonekana kufanya vizuri kwenye masomo yao na kubainisha kuwa huenda wangeachwa na kuendelea kusishi maisha magumu ingekuwa mwanzo wa kuharibu vipaji vyao.

Share To:

Post A Comment: