Timu ya mpira wa miguu ya ILEMI FC imeibuka mshindi wa Fainal za Tulia Trust Uyole Cup dhidi ya wapinzani wao ZARAGOZA FC iliyowatoa kwa mikwaju ya penati katika Viwanja vya Mwawinji, Uyole ya kati huku ikishuhudiwa na Viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homela ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi.


Viongozi wengine walioshuhudia mtanange huo ni pamoja na Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson, Meya wa Jiji la Mbeya Jiji Dourmohamed Issa, Mkurugenzi wa Rapha Group Raphael Ndelwa


Ukiachilia mbali zawadi za makundi mbalimbali, Team shindani zimepewa zawadi ikiwemo Mshindi wa Tatu kupewa Milioni moja, Mshindi wa Pili Milioni Mbili na Mshindi wa kwanza ameibuka na kitita cha Shilingi milioni tatu.

Share To:

Post A Comment: