Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya amewataka mafundi wanaotekeleza miradi  ya EP4R katika Halmashauri hiyo kuwa na kasi ya ujenzi wa miradi hiyo bila kuathiri uimara .

Mwl.Makwinya ameelekeza  hayo wakati wa ziara yake  katika Shule ya Msingi Kisimiri chini,Kata ya Uwiro ambapo ujenzi wa mradi wa vyumba viwili vya Madarasa ya EP4R umeonekana  kuwa wa polepole kutokana na fundi kutokuwa na Nguvu kazi ya kutosha na kutokuwepo eneo la mradi .

Aidha, Mwl.Makwinya ameuelekeza Uongozi unaosimamia  ujenzi huo kutafuta Suluhu Mara moja ili mradi huo kukamilika kwa wakati kama ilivyokusudiwa.

Vilevile Makwinya  alitembelea na kupongeza  ari ya ujenzi  wa vyoo vya matundu 12 vya muundo wa  SWASH katika Shule hiyo pamoja na mradi wa uchimbaji Maji yatakayo sambazwa kwenye Shule ya Sekondari Kisimiri.

Diwani wa Kata ya Uwiro Mhe.Dauson Urio ameishukuru Serikali kupeleka miradi ya vyumba vya Madarasa mawili ya EP4R na Vyoo hivyo vya matundu 12 ,pia amehimiza Kazi za ujenzi wa miradi kutolewa kwa mafundi wanaojituma zaidi.

Kata ya  Uwiro ni Miongoni mwa Kata saba(7) ambazo  Mkurugenzi Zainabu amefanya ziara ya kukagua  na  kutembelea utekelezaji wa  miradi ya EP4R ,Miradi ya Nguvu za wananchi na michango ya wahisani,miradi ya TASAF pamoja na maboma ya mda mrefu ,ambapo aliambatana na Afisa Elimu Sekondari  pamoja na Wahandisi wa Ujenzi toka  Halmashauri.


Share To:

Post A Comment: