Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof. James Mdoe, akivishwa Skafu na vijana wa Shule ya Sekondari Kihesa baada ya kuwasili shuleni hapo kwa ajili ya kukagua mradi wa kukuza ujuzi wa matumizi ya Kompyuta kwa wanafunzi wa shule za Sekondari mkoani Iringa unaoendeshwa na Shirika la Global - Outreach Tanzania la mjini Iringa kupitia ufadhili wa Mfuko wa Kukuza Ujuzi (SDF) unaosimamiwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof. James Mdoe katika picha ya pamoja na maafisa wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) na wale wa Global - Outreach Tanzania alipotembelea ofisi za Shirika hilo la mjini Iringa. Shirika hilo linaendesha mradi wa kukuza ujuzi wa matumizi ya Kompyuta kwa wanafunzi wa shule za Sekondari mkoani Iringa kwa ufadhili wa Mfuko wa Kukuza Ujuzi (SDF) unaosimamiwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof. James Mdoe akiwa katika chumba cha Kompyuta katika Shule ya Sekondari Ihesa mkoani Iringa ambayo ni  miongoni mwa shule sita zilizonufaika na mradi wa kukuza ujuzi wa matumizi ya  Kompyuta kwa wanafunzi wa shule za Sekodari mkoani Iringa kupitia ufadhili wa Mfuko wa Kukuza Ujuzi (SDF) unaosimamiwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania(TEA).

Wanafunzi wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari Kihesa mkoani Iringa wakimskiliza Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof. James Mdoe alipotembelea shule hiyo kwa ajili ya kukagua mradi wa kukuza ujuzi wa matumizi ya Kompyuta kwa wanafunzi wa shule za Sekondari mkoani Iringa kwa ufadhili wa Mfuko wa Kukuza Ujuzi (SDF) unaosimamiwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).

Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari Kihesa mkoani Iringa wakiwa katika chumba cha Kompyuta ambacho ni sehemu ya mradi wa kukuza ujuzi wa matumizi ya  Kompyuta kwa wanafunzi wa Sekondari mkoani Iringa unaoendeshwa na Shirika la Global- Outreach Tanzania kupitia ufadhili wa Mfuko wa Kukuza Ujuzi (SDF) unaosimamiwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania(TEA).

*********************************

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof. James Mdoe amekumbusha wanafunzi walioko mashuleni kusoma kwa malengo na kuyafanyia kazi kwa bidii na nidhamu ili kufanikisha ndoto zao za kitaaluma badala ya kusoma kwa mazoea.

Akizungumza na wanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari Kihesa, mkoani Iringa, Prof. Mdoe amesisitiza kuwa mafanikio ya wanafunzi yatatokana na wao kujua wanataka nini katika maisha pamoja na kuweka bidii ya kufanikisha  malengo hayo. Ametoa mfano kwa wale wanaotaka kuwa Madaktari au Wahandisi lazima wafanye vizuri katika masomo ya Sayansi.

Ametumia fursa hiyo kuwahimiza wanafunzi hao kuwa na mawazo ya kijasiriamali yatawawezesha kujiajiri badala ya kutegemea kuajiriwa pindi wanapohitimu masomo “hata kama unataka uingie mtaani lazima ujue unaenda kufanya nini” amesema Prof. Mdoe.

Naibu Katibu Mkuu huyo, amezungumza na wanafunzi hao ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kutembelea taasisi tano kati ya 81 zinazonufaika na ufadhili wa Mfuko wa Kukuza Ujuzi (SDF) unaoratibiwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).

Shule ya Sekondari Kihesa ni miongoni mwa shule sita za Sekondari mkoani Iringa zinazonufaika na mradi wa kukuza ujuzi wa matumizi ya Kompyuta kwa wanafunzi wa shule za Sekondari mkoani Iringa unaoendeshwa na Shirika la Global Tanzania kwa ufadhili wa Mfuko wa Kukuza Ujuzi (SDF) unaosimamiwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Global Outreach Tanzania, Maryline Mamuya ameishukuru Serikali kwa kutoa ufadhili kupitia Mfuko wa SDF ambao  unaowezesha shule sita za sekondari mkoani Iringa kupata elimu ya matumizi ya Kompyuta ambayo ni muhimu  katika zama hizi za kidijitali.

Aidha Naibu Katibu Mkuu ametembelea na kuzungumza na wanufaika wa mradi wa kukuza ujuzi katika usindikaji wa mazao na stadi za ujasiriamali, unaoendeshwa na Shirika la Kuendeleza Viwanda Vidogo Nchini (SIDO) mkoani Singida ambao pia umefadhiliwa na Mfuko wa Kukuza Ujuzi.

Akiwa SIDO amekutana na kuzungumza na wanufaika wa  mafunzo hayo pamoja  na kujionea bidhaa zinazotengenezwa na wanufaika hao ambao baadhi yao wamefanikiwa kupata usajiri wa nembo  ya ubora wa TBS baada ya kupata mafunzo hayo yaliyofadhiliwa na SDF

Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF) ni Mfuko unaolenga kuwezesha Taasisi zinazotoa mafunzo kuongeza ubora na ufanisi katika kutoa mafunzo ya ujuzi na stadi za kazi katika sekta sita za kipaumbele nchini ambazo ni Kilimo - Uchumi, Utalii na Huduma za Ukarimu, Uchukuzi, Ujenzi, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na Nishati.

Taasisi 81 zimenufaika na awamu ya pili ya Mfuko wa SDF ambapo kiasi cha Shilingi Bilioni 9.7 zinatumika katika ufadhili huo. Mamlaka ya Elimu Tanzania imepewa jukumu na kuratibu utekelezaji wa Mfuko huo.

Share To:

Post A Comment: