Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb) akiiagiza Menejimenti ya Benki ya TPB kuangalia namna itakavyo punguza riba za mikopo ili kuchochea biashara na shughuli nyingine za maendeleo kwa wananchi, katika ziara yake ya kutembelea taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb), akikabidhiwa kitabu na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB, Bw. Sabasaba Moshingi, alipotembelea Benki hiyo katika ziara yake ya kutembelea taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dar es Salaam.


Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb), akiongoza mkutano wa Menejimenti ya Benki ya TPB, katika ziara yake ya kutembelea taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam.


Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB, Bw. Sabasaba Moshingi, akieleza hatua mbalimbali ambazo Benki hiyo imechukua katika kuhakikisha inaimarika, wakati wa mkutano wa Menejimenti ya Benki hiyo na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb) (hayupo pichani), jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi wa Mikopo wa Benki ya TPB, Bw. Henry Bwogi, akieleza namna Benki hiyo ilivyojidhatiti kutoa mikopo kwa wanachama wake katika kutekeleza adhima ya Serikali ya kuwaletea maendeleo wananchi wake, wakati wa ziara Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb) (hayupo pichani) ya kutembelea taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB, Bw. Sabasaba Moshingi (katikati), akimuonesha Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb), baadhi ya viongozi waliopita wa Benki hiyo, wakati wa ziara ya Naibu Waziri huyo katika taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango.


Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb) akiongoza kikao cha viongozi wa tasisi ya Soko la Bidhaa Tanzania (TMX), alipotembelea taasisi hiyo, jijini Dar es Salaam.


Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Bidhaa Tanzania (TMX) Bw. Godfrey Malekano, akieleza jambo wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb) (hayupo pichani), jijini Dar es Salaam.


 Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Soko la Bidhaa Tanzania (TMX), Bw. Augustino Mbulumi, akieleza namna wanavyofanya minada kwa njia ya kidigitali, wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb) (hayupo pichani), alipotembelea Soko hilo, jijini Dar es Salaam


Picha ya namna Soko la Bidhaa Tanzania (TMX) linavyofanya kazi.

Share To:

Post A Comment: