Mkuu wa Wilaya ya Lushoto ndugu Kalisti Lazaro leo Jumatano tarehe 30/06/2021 amekutana na Wakuu wa Taasisi za Serikali zilizopo Wilayani Lushoto.


Kikao hicho kilihudhuriwa na Mameneja wa Wilaya kutoka Taasisi zifuatazo:-RUWASA, MABUGHAI CDTI, DS QAO Lushoto, TTCL, LUWIUSA, TRA, TARURA, NMB, NIDA, NSSF, TANESCO, POSTA, TAFORI, TSF


Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Lushoto alihaidi kuzipa Ushirikiano Taasisi hizo na aliwasisitiza Wakuu wa Taasisi hizo kufanya kazi kwa Ueledi, Bidii ili kutatua Kero za Wananchi wa Wilaya ya Lushoto na kudumisha Mshikamano na Ushirikiano miongoni mwa Taasisi hizo.


Wakuu wa Taasisi hizo walimpongeza Mkuu wa Wilaya ya Lushoto kwa Kuaminiwa na Kuteuliwa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan na kuhaidi kumpa ushirikiano katika kutekeleza Majukumu yake ya kuwatumikia Wananchi wa Wilaya ya Lushoto

Share To:

msumbanews

Post A Comment: