Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Kalisti Lazaro leo amezindua Zoezi la Uhamasishaji wa Bima ya Afya - CHF Iliyoboreshwa (Improved Community Healthy Fund - ICHF) lililofanyika KiWilaya katika Kata ya Mlalo & Kwemshasha Tarafa ya Mlalo.


Katika zoezi hilo Mkuu wa Wilaya ya Lushoto ndugu Kalisti Lazaro aliambatana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Lushoto ndg Mathew Paulo Mbaruku, Diwani wa  Kata ya Lunguza  na Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii (Kamati ya Elimu, Afya, Maji) ndg Yasini Billa, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto ndg Tadeo Simon Kachenje, Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto ndg Esuphati Kivuyo, Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya (DMO) ndugu Gasto S Laswai, Mkurugenzi wa Improving Tanzania Foundation (ITF) ndugu Henrish Madambo, Mratibu wa Improved Community Healthy Fund (ICHF) Mkoa wa Tanga ndugu Imani Clemence na Maneja wa NMB Tawi la Lushoto ndugu Benadeta Mbuya


Mkuu wa Wilaya aliwahasa Wakazi wa Tarafa ya Mlalo kujiunga kwa wingi kwenye Mfuko wa Bima ya Afya Iliyoboreshwa (CHF) ili waweze kupatiwa Matibabu bure kwenye Zahanati, Vituo vya Afya, Hospitali ya Wilaya na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa


Mkuu wa Wilaya Lushoto ndugu Kalisti Lazaro alieleza kuwa Mfuko huu umeboresha huduma zake kwani kwa sasa hudhuma za kupata Matibabu zimeboreahwa kutoka ile ya awali (CHF) ambayo huduma zilikuwa zinatolewa kwa Wilaya husika tu kwa sasa Mteja aliyejiandikisha kwenye ICHF atapata huduma kuanzia ngazi ya Zahanati hadi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa aliongeza kuwa Serikali tunasimamia Uhakiki wa upatikanaji wa Huduma Bora za Afya katika Vituo vyote vya kutolea huduma za Afya.


Pia aliwasihi Wazazi kuhakikisha Watoto ambao wako Mashuleni wanakatiwa Bima ya Afya kwani Wanafunzi wanaweza kujiunga kwa Makundi kwa kuchangia kiasi cha Tsh 5,000/= kwa kila Mwanafunzi na kutengeneza Idadi ya Wanafunzi 6 kwa kila Kundi.


Pia Mkuu wa Wilaya aliwashukuru Wadau wa Maendeleo ambao wameshirikiana na Serikali kuhakikisha utekelezaji wa Mpango huu unaendelea. Shirika la Improving Tanzania Foundation (ITF) limewasaidia Watoto 100 waishio katika mazingira hatarishi kupata Bima ya Afya Iliyoboreshwa*


*Kampeni hii ilikuwa na kauli mbiu ya "CHF ILIYOBORESHWA KWA AFYA YA KILA MTANZANIA , JIUNGE LEO" na lengo ni kuzifikia  asilimia 30% ya Kaya katika Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto na mpaka sasa Kaya 2,400 tayari zimejiunga na Mfuko wa Bima ya Afya iliyoboreshwa sawa na asilimia 3.4%*

Share To:

msumbanews

Post A Comment: