Na Lulu Mussa Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.Selemani Jafo amewaagiza wamiliki wa kumbi za starehe na burudani kuhakikisha sauti zitokanazo na shughuli zao hazizidi viwango vinavyokubalikakwa mujibu wa sheria.
Waziri Jafo amesema hayo hii leo Jijini Dodoma wakati wa kutoa Tamko kwaumma juu ya udhibiti wa uchafuzi wa mazingira utokanao na kelele na mitetemona kuwaagiza wamiliki wa maeneo ya burudani na starehe kuzingatia matumizi ya vipima kelele na vizuia sauti kama ilivyoelekezwa kwenye masharti yote ya leseni zao.
“Katika kuhakikisha tunalinda Afya ya Jamii kutokana na athari zitokanazo nakelele na mitetemo Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira, kwakushirikiana na Ofisi ya Rais – TAMISEMI; Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji;Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto; Wizara yaViwanda na Biashara; Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi; Wizara yaElimu, Sayansi na Teknolojia; Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi; na Wizara yaHabari, Sanaa na Michezo tunaelekeza Kila Mwananchi ahakikishe shughulianazofanya hazisababishi kero ya kelele na mitetemo” Jafo alisisitiza.
Aidha, Waziri huyo amesema kasi ya ukuaji wa uchumi inaenda sambamba naongezeko la shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii ambazo zinaambatanana ongezeko la uchafuzi wa mazingira unaotokana na Kelele na Mitetemo nakusababisha athari za kiafya na kimazingira kwa jamii.Aliongeza kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa ya maendeleo katika Nyanja zakiuchumi na kijamii kutokana na Mipango madhubuti ya Serikali kwenyeUwekezaji katika Sekta mbalimbali.
Hivyo, ameutaka umma wa Watanzania kuhakikisha agenda ya kelele namitetemo inakuwepo kwenye mikutano ya wakazi na kuwaomba wananchi kutoataarifa kuhusu kero na mitetemo kwa Ofisi za Serikali za Mitaa au NEMC kwaNamba za bure (0800110115 au 0800110117 au 0800110116)Amesema yeyote atakayesababisha kero zitokanazo na kelele na mitetemokinyume na Kanuni za Usimamizi wa Mazingira (Udhibiti wa kelele na mitetemo)za mwaka 2015 atakuwa amevunja sheria na adhabu yake ni faini isiyopunguashilingi milioni moja au kifungo kisichozidi miezi sita, sambamba na kufungiwakwa biashara husika.
Kwa upande mwingine Waziri Jafo ametoa rai kwa viongozi wa Dini kupitia Kamati za Amani, kulijadili suala hili la Kelele na Mitetemo iliyopitiliza kutoka kwabaadhi ya nyumba za ibada ili kupata namna bora ya kuendesha ibada kwamaslahi mapana ya afya ya jamii.
Nae Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. DorothyGwajima amesema wataendelea kuelemisha jamii juu ya athari za kiafyazitokanazo na kelele na mitetemo iliyopitiliza ili kuwa na jamii yenye afya bora nakupunguza gharama za matibabu kwa Serikali.
Waziri Jafo aliambatana na Waziri wa Afya, Mandeleo ya Jamii, Jinsia na WatotoMhe. Dorothy Gwajima, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu WenyeUlemavu Mhe. Ummy Nderiananga; Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Sayansi naTeknolojia Mhe. Omary Kipanga; Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani yaNchi Mhe. Khamis Chillo; na Naibu Waziri Wizara ya Habari, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul
Post A Comment: