Na Angela Msimbira DAR-ES-SALAAM


Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amewaagiza Wakurugenzi wa Halmsahauri zote nchini kuhakikisha wanapanga bajeti ya kufanyia matengenezo magari ya Halmashauri ili yaweze kudumu kwa muda mrefu

Akizungumza na Maafisa Elimu wa Halmashauri ya zote 184 Nchini wakati wa Uzinduzi wa zoezi la ugawaji wa  Magari  kwa maafisa  hao yaliyonunuliwa kupitia mradi wa lipa kulingana na matokeo mapema leo katika Viwanja vya Shule ya Sekondari  ya Kibasila  Mkoani Dar-es-salaam


‘Kuna baadhi ya Halmashauri hazitengi bajeti  kwa ajili ya matengenezo ya magari yao , na kusababisha  magari hayo kuharibika mapema na kuwekwa Gereji bila matengenezo  ya Halmashauri zao


“Maafisa elimu wa Wilaya Mkikabidhiwa magari haya leo na tukalikuta gari limekaa na halifanyi kazi kwa kukosa matengenezo lazima Wakurugenzi wa Halmashauri watawajibishwa “ amesisitiza Majaliwa


Amesema kila Halmashauri lazima iweke mpango wa matengenezo wa magari hayo ili ziweze kufanyakazi  kwa muda mrefu  na kuweza kufamnya kazi iliyopangiwa ya kuhakikisha inafanya ufutiliaji wa elimu katika shule za msingi nchini.


Amefafanua kuwa magari hayo yatumike kwa ajili ya ufuatiliaji wa miradi ya ujenzi wa miundombinu ya elimu katika Halmashauri na kuhakikisha yanafuatilia ufundishaji na ujifunzaji wa elimu katika Wilaya ili malengo yaweze kufikika na kukamilika kwa wakati


Amewaagiza Wakuu wa Mikoa na Wilaya  kuwachukulia hatua  maafisa Elimu wote ambao watayatumia magari hayo kinyume na kazi iliyopangiwa ya ufuatiliaji wa masuala ya Elimu katika Halmashauri  kwa kuwa watakuwa wameenda kinyume na matakwa ya Serikali 


Hata hivyo, amewaagiza maafisa elimu wote nchini kuhakikisha wanafanyakazi kwa weledi kwa kuwa ndio msingi wa mafanikio katika maeneo yao kwa kuwa kiwango cha mafanikio ya elimu kilichofikiwa bado kinahitaji nguvu zaidi ili tuweze kufik mbali zaidi.


‘Tunatambua changamoto zinazoendelea katika Halmashauri zenu na Serikali inatambua umuhimu wa elimu niwatake muendelee kufanyakazi kwa weledi na uaminifu ili kuongeza ufaulu na Serikali itaendele kutatua changamoto zenu’amesisistiza Majaliwa


Amewataka kuhakikisha wanawatia moyo waalimu katika kutekeleza majukumu yao , watembeleeni, wasikilizeni na  wahudumieni kwa kufuata sheria na taratibu za  utumishi wa umma  na imarisheni mahusiano katika utendaji kazi wa kila siku ili kufikia malengo yaliyowekwa na Serikali ya kuongezaufaulu kwa wanafunzi.


Aidha ametaka Maafisa Elimu Nchini kuwatumia Madiwani  katika kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa elimu kwa watoto na kuhakkisha wazazi wanawajibika katika suala zima la kutimiza majukumu yake katika kuhakikisha watoto wanapata elimu bora


Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu  amesema   magari hayo  yamenunuliwa na Serikali  kupitia Programu ya Lipa Kulingana na Matokeo kwa  gharama ya shilingi  bilioni 16.4.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: