NA ANDREW CHALE


Mbunifu nguli wa mitindo ya mavazi nchini Mustafa Hassanali  amesema kwa kushirikiana na wabunifu wengine hapa nchini wanatarajia kumbunia vazi maalum  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan.


Mustafa ambaye pia ni Mwenyekiti wa  Chama cha wabunifu yaani Fashion Association of Tanzania (FAT) amesema hayo wakati wa utoaji wa tuzo za msimu wa kwanza za Harusi (Wedding Awards 2021) zilizofanyika Serena Dar es Salaam.


"Mimi hili la kumbunia vazi Rais wetu Mama Samia nimelichukua na nitahakikisha nalivalia njuga.


Tumeshuhudia Mama Samia akiwa gumzo huko Kenya na mitandaoni kutokana na mavazi yake" Alisema Mustafa Hassanali.


Mustafa Hassanal aliongeza kuwa, kwa wastani Mama anaweza kuvaa nguo tofauti zaidi ya 3 hadi 4 hivyo mara miaka minne  iliyobakia wabunifu wanaweza kumshonea nguo zaidi ya 6000.


"Mimi Mwenyekiti wa Wabunifu wote Tanzania nitahawamasisha tukashona vazi la ubunifu kisha tukampelekea, akilipenda litanunuliwa utapata kipato na ikatokea hajalipenda basi tuendelee kubuni zaidi" alisema Mustafa Hassanali.


Aidha alisema wabunifu wengi wakubwa wamekuwa wakipata kipato kupitia mavazi yao wanayobuni kwa viongozi ikiwemo mbunifu wa anayembunia Mama Michelle Obama.


Awali katika usiku huo wa tuzo za Harusi, Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Taasisi ya sekta binafsi nchini (TPSF), Bi. Angelina Ngalula aliwataka watu wa sekta ya Harusi kuwa na umoja wao madhubuti ambao utaleta faida kubwa kwao na Taifa.


"Tanzania bado hatujafikia malengo katika sekta hii ya harusi. Hii ni dhahabu nyeupe, Almasi nyeupe bado ipo chini haijachimbwa nakupongeza sana Mustafa Hassanal kwa kuja na wazo hili.


Pia washindi na ambao hawakubahatika kushiriki ninaamini kuwa mshiriki ni ushindi tosha na inaongeza juhudi kwa kujipanga wakati ujao" alisema Bi. Angelina Ngalula.


Aidha, alibainisha kuwa, Sekta ya Harusi itafanya makubwa siku za usoni endapo itachukuliwa kwa mapana yake.


"Mustafa Hassanali   Tanzania tumebahatika kumpata Rais Mwanamke Mama yetu Mhe. Samia Suluhu Hassan. Nyie kama wabunifu ebu fanyeni kitu basi kisha mkamkabidhi huo ubunifu wenu..nawaachia hilo" alisema.


Hata hivyo aliwataka watu wa harusi kuwa na forum yao ambayo itasaidia kuwa na takwimu sahihi katika shughuli zao na sekta nzima.


"Kenya wanaingiza Bilioni 30 fedha ya Kenya kwa mwaka kutokana na sekta ya Harusi pekee ambapo wanakuwa na harusi zaidi ya 28,000 kwa mwaka tu, lakini hapa kwetu hatuna hiyo takwimu hivyo basi mkichukue na hili mlifanyie kazi" Alisema.


Aidha, aliwataja kuhakikisha Tanzania wanatumia vivutio vilivyopo ilikuwa sehemu ya kuvutia harusi za kimataifa ambapo wageni wanaweza kutoka mataifa mengine na kuja kufunga ndoa Tanzania.


Aidha katika tuzo zilizoandaliwa na Kampuni ya 361 Degrees ya Dar es Salaam awali ilikuwa na jumla ya washiriki Sitini na tano (65) wakiwania tuzo hizo katika vipengele Ishirini (20) ni pamoja na: 


Tuzo ya Harusi ya Bridal hair & Make-up artist  of the year imeenda kwa Zuu Make-up studio (Bukoba), Henna artis of the Year imeenda kwa Hennah Creations Tanzania, Jewellery store of the year imeenda kwa Sabena Jewellery, Life time Archievement  of the Year, imeenda kwa Maznat Sinare, Pre-wedding mentor [somo] of the year imeenda kwa Rosemary Mizizi.


Washindi wengine ni 

Wedding accessories store of the year imeemda kwa Delightful Wedding, Wedding cake bakaer of the year imeenda kwa Jasthers cakes and Connectionery  (Arusha), Wedding catere and desert maker of the year imeenda House of Pastries, Menswear designer of the year imeenda kwa Martin Kadinda.


Pia Wedding floriest of the year imeenda kwa Blossom TZ, Wedding gown designer and Boutique of the year imeenda kwa Fifi sugar design, Wedding MC of the year imeenda kwa MC Tully, Wedding transport provider of the  year imeenda kwa Motto cars, Weddig venue of the year imeenda kwa Mbezi Beach Executive hall, Wedding Salon/Spa ofe the year imeenda kwa The Touch Spa, Wedding set and decor of the year imeenda kwa Mama Events TZ (Arusha).


Wedding Photographer of the year  imeenda kwa JKM, Wedding stationey Supplier of the year imeenda kwa Orbit cards  and gift shop (Arusha), Wedding Videographer of the year imeenda kwa iSTUDIO, Bridal Boutique of the year imeenda kwa Almanito Wedding na Wedding of the Year  imeenda kwa Haji Manara.


Share To:

msumbanews

Post A Comment: