Na Imma Msumba, Mwanga 

 Wanawake wa Halmashauri ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro wametakiwa kutumia vizuri mikopo yao kwa kuwekeza kwenye shughuli  mbalimbali za maendeleo na zitakazo zalisha kwa wingi na kuwaletea mapato yakutosha katika familia zao.

Ameyasema hayo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mwanga  Mhe.Saleh Mkwizu alipokutana na vikundi vya kina mama wajasiriamali wadogo wadogo waliojiajiri katika masoko na minada katika Kata mbalimbali za Halmashauri hiyo.

Mhe. Mkwizu amewataka wanawake hao kuonyesha kuwa wanaweza kuinuka kiuchumi na kuacha utegemezi huku wakitekeleza majukumu yao katika ngazi za familia na jamii kwa ujumla.

“Mikopo hiyo mnayoenda kupewa ichukulieni kama mmepata tunda la embe katika mti wa miba,mkaitumie vizuri  mikopo hiyo na muache kwenda kununua vitu ambavyo havitawasaidia katika kujiletea maendeleo yenu na familia zenu"

Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wetu mpendwa mama Samia Suluhu Hassan imelenga katika kuhakikisha matunda ya nchi yanaliwa na kila mtanzania,hivyo fursa hiyo ya wanawake kupatiwa mitaji kwa mikopo isiyo na riba nimkakati mzuri wakuendelea kutelekeza Ilani ya Chama cha Mapinduzi.

Halmashauri yangu ipo tayari kuwasaidia wakimama wote watakao fanikiwa kumaliza marejesho yao na nitawasaidia kupata mikopo mingine ya riba nafuu huku mkiwa katika vikundi vyenu,pia muendelee kutafuta fursa kubwa zaidi katika miradi mikubwa inayofanywa na serikali,ili muweze kukua katika biashara zenu.

Pia nipende kuipongeza Idara ya Maendeleo ya Jamii kwa juhudi wanazozifanya za kusaida makundi maalumu ya vijana,wanawake na wenye ulemevu katika Halmashauri ya Mwanga.

Niwasihi wadau wa maendeleo Wilaya ya Mwanga na wenye mapenzi mema kwa Halmashauri yetu waendelee kusaidia akinamama katika nyanja ya kujikwamua kiuchumi ile pale wanapokosa usaidizi basi waweze kusimama wao kama wao na kuendesha maisha yao na wategemezi wao.


Share To:

msumbanews

Post A Comment: