Afisa udhibiti ubora, Mhandisi Emmanuel Shilinde (TBS) akimweleze mfanyabiashara wa duka umuhimu wa kusoma taarifa katika vifungashio na kununua bidhaa zilizothibitishwa ubora wake na TBS kwa mfanyabiashara wa mikate wa eneo la Kayanga mjini, wilayani Karagwe mkoa wa Kagera. Afisa udhibiti ubora, Mhandisi Emmanuel Shilinde (TBS) akiwaelezea muuzaji wa vyakula umuhimu wa kusoma taarifa katika vifungashio na kuuza bidhaa zilizothibitishwa ubora wake na TBS kwa wafanyabiashara wa mikate wa eneo la Omuroshaka, wilayani Karagwe mkoa wa Kagera.
Diwani wa kata ya Bugene wilayani Karagwe-Kagera Mhe. Mugisha Mathias akizungumza mara baada kukutana na maafisa wa TBS baada ya kutembelea katika kata hiyo wakati wa kampeni ya elimu kwa umma katika ngazi ya wilaya iliyokuwa inafanyika kanda ya ziwa,Diwani wa kata ya Bugene wilayani Karagwe-Kagera Mhe. Mugisha Mathias akiwana baadhi ya viongozi wa kata hiyo wakipata picha ya pamoja na baadhi ya maafisa wa TBS
Wanafunzi wa shule ya msingi Kayanga na Rumanyika, wilayani Karagwe- Kagera wakisikiliza kwa makini elimu ya viwango kutoka kwa Afisa masoko mwandamizi wa TBS, Bi. Gladness Kaseka ili wawe mabalozi wazuri wa masuala ya viwango katika kaya zao kwa miaka ijayo.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Bugene, wilayani Karagwe- Kagera wakisikiliza kwa makini elimu ya viwango kutoka kwa maafisa wa TBS ili wawe mabalozi wazuri wa masuala ya viwango katika jamii zao.
Shirika la Viwango Tanzania TBS limeendelea na zoezi lake la kutoa elimu ya viwango vya ubora wa bidhaa na Chakula kwa wafanyabiashara, mashuleni pamoja na wananchi kwa ujumla wilayani Karagwe mkoani Kagera.
Diwani wa kata ya Bugene wilayani Karagwe Mhe.Mugisha Mathias ameipongeza TBS kwa elimu ambayo wanaitoa katika wilaya hiyo kwani kuna baadhi ya wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla hawakuwa na elimu ya ubora wa bidhaa kwa undani zaidi.
"Naipongeza TBS kwa kazi nzuri wanaoifanya na natoa wito waendelee na kasi hiyohiyo ya utendaji". Amesema Mhe. Mathias.
Post A Comment: