Makamu Mkuu wa Chuo-Taaluma Dkt. Momole Kasambala akizungumza katika Kikao cha Baraza Kuu la Nne la Wafanyakazi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA)  kilichofanyika Ukumbi wa  Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine ( SUA)  mkoani Morogoro leo Machi 29, 2021.
Mwakilishi wa Meneja Rasilimali Watu  TIA, John Gama, akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake (RAAWU), TIA,  Kampasi ya Singida, Seba Ernest, akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Mjumbe wa kikao hicho, Alton Kanjolonga kutoka Kampasi ya Singida, akichangia jambo kwenye kikao hicho.

Wajumbe wa baraza hilo wakiwa kwenye kikao hicho.

Kikao kikiendelea.

Wajumbe wa baraza hilo wakiwa kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea. Na Mwandishi Wetu, Morogoro


MAFUNZO kwa njia ya mtandao ambayo yanatarajiwa kutolewa na Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) yatawanufaisha wananchi wengi.

Hayo yamebainika katika Kikao cha  Baraza Kuu la Nne la Wafanyakazi wa TIA kilichofanyika jana Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine ( SUA)  mkoani Morogoro.

Wajumbe wote kabla  ya kuanza kikao hicho  walisimama kwa dakika moja ikiwa ni ishara ya kumkumbuka aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt.John Pombe Magufuli.

 Akizungumza katika kikao hicho Makamu Mkuu wa Chuo-Taaluma Dkt. Momole Kasambala alisema mafunzo hayo yanatarajia kuanza pindi utakapo kamilika utafiti wao na kuwa yatatoa fursa kwa wananchi wengi kuyapata.

"Tupo kwenye mchakato wa kuanza kutoa mafunzo haya na tukisha kamilisha kufanya utafiti wetu tutaanza kuyatoa wakati wowote." alisema Kasambala.

Kasambala akizungumzia mahusiano ya chuo hicho na vyuo vingine alisema   kitaanzisha mahusiano na 
ushirikiano na vyuo vya ndani na nje ili kubadilishana uzoezi wa ufundishaji.

" Hivi sasa tunaandaa  maridhiano ya pamoja baina yetu na Chuo Kikuu cha Irkutsk cha Urusi ili kuanzisha ushirikiano huo." alisema Kasambala.

Alisema katika kikao chao cha maazimio cha mwaka jana  waliazimia kuingia mikataba na baadhi ya taasisi za kifedha kama benki ya Posta, CRDB na NMB kwa ajili ya kuwakopesha wafanyakazi wao riba nafuu ambapo tayari Benki ya NMB imefanya mkataba nao ambapo riba yao ni 15%.
Share To:

Post A Comment: