Mwenyekiti wa Kikao cha  Baraza Kuu la Nne la Wafanyakazi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA)  Profesa Carolyne Nombo, akiongoza kikao hicho kilichofanyika Ukumbi wa  Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine ( SUA)  mkoani Morogoro ambacho kilikuwa na ajenda 11. Kulia ni Naibu Katibu wa Baraza hilo, Halima Muhsin.

Katibu Mkuu Taifa wa Chama chama cha Wafanyakazi (RAAWU), Winstone Makele, akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Mwanasheria wa TIA, Said Mayunga akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Wajumbe wa baraza hilo wakiwa kwenye kikao hicho.
 Wajumbe wa kikao hicho wakiongozwa  na Mwenyekiti wao Profesa Carolyne Nombo (kushoto) wakiwa wamesimama kwa dakika moja ikiwa ni ishara ya kumkumbuka aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt.John Pombe Magufuli.
Wajumbe wakiwa wamesimama kwa dakika moja ikiwa ni ishara ya kumkumbuka aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt.John Pombe Magufuli.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Uhusiano TIA, Lillian Rugaitika,akichangia jambo kwenye kikao hicho.

Mwenyekiti wa kikao hicho,  Profesa Carolyne Nombo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine. Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Taifa wa Chama chama cha Wafanyakazi (RAAWU), Winstone Makele, Makamu Mkuu wa Chuo Mipango, Fedha na Utawala,  Dkt. Modest Assenga, Makamu Mkuu wa Chuo-Taaluma Dkt. Momole Kasambala  na Naibu Katibu wa Baraza hilo, Halima Muhsin.
Picha ya pamoja. Na Dotto Mwaibale, Morogoro


TAASISI ya Uhasibu Tanzania (TIA) inatarajia kuanza kutoa mafunzo kwa njia ya mtandao ili kuwanufaisha watanzania.

Hayo yalielezwa katika Kikao cha  Baraza Kuu la Nne la Wafanyakazi wa TIA lililoketi Ukumbi wa  Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine ( SUA)  mkoani Morogoro ambacho kilikuwa na ajenda 11.

Kabla ya kuanza kikao hicho wajumbe wote wakiongozwa  na Mwenyekiti wao Profesa Carolyne Nombo walisimama kwa dakika moja ikiwa ni ishara ya kumkumbuka aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt.John Pombe Magufuli.

 Akizungumza katika kikao hicho Profesa Carolyne Nombo alisema mafunzo hayo yataanza kutolewa hivi karibuni.

"Tupo kwenye mchakato wa kuanza kutoa mafunzo haya na tukisha kamilisha kufanya utafiti tutaanza kuyatoa mapema iwezekanavyo." alisema Nombo.

Makamu Mkuu wa Chuo-Taaluma Dkt. Momole Kasambala akizungumzia ajenda nyingine alisema chuo hicho kitaanzisha mahusiano na ushirikiano na vyuo vya ndani na nje ili kubadilishana uzoezi wa ufundishaji na mambo mengine na tayari wapo katika hatua ya kuandaa maridhiano ya pamoja baina yao na Chuo Kikuu cha Irkutsk cha Urusi ili kuanza rasmi kushirikiana katika nyanja kadhaa zitakazoainishwa kwenye mkataba huo.

Alisema katika maazimio ya kikao cha baraza hilo la mwaka jana waliazimia kuingia mikataba na benki za Posta, CRDB na NMB lengo likiwa ni kuongeza wigo wa mikopo yenye riba nafuu kwa wafanyakazi ambapo tayari wamekwisha fanya mkataba na Benki ya NMB kwa riba ya asilimia 15.

Share To:

Post A Comment: