Mbunge wa Mbeya Mjini ambaye pia ni Naibu Spika Dr. Tulia Ackson ameahidi kuchangia mifuko 200 ya saruji katika shule ya Sekondari Iganzo mara baada ya kuwakuta Wananchi wa kata hiyo wakichangishana fedha kwa lengo la kujenga madarasa sita kwa kushirikiana na Serikali kutokana na kuwepo kwa changamoto ya madarasa katika shule hiyo.


Dr. Tulia amesema>>>”Nimeelezwa hapa kwamba mmekuwepo hapa tangu asubuhi na mmeamua kujichangisha wenyewe ikiwemo kusimamia ujenzi huu wa madarasa, binafsi ninawashukuru sana na kuwapongeza kwamaana ingeweza kukataa hili wazo la kuchangia mliloamua kulifanya kwa kushirikiana na Serikali”- ”-Dr. Tulia Ackson


“Niwaahidi tu kwamba kwa utayari wenu huu basi niwaahidi tutashirikiana kwa pamoja hadi kuhakikisha shughuli hii imekamilika, nafahamu kwamba changamoto hizi zipo sehemu nyingi hususani hapa kwetu Mbeya mjini, nimshukuru pia Mkurugenzi wetu wa jiji ambaye naye ameonesha utayari wa kutusaidia fedha”- ”-Dr. Tulia Ackson


“Msiwe na wasisiwasi madarasa haya tutajenga kwa pamoja na kwa kuanzia mimi nitaleta hapa mifuko 200 ya saruji na hii italetwa kesho na bado tutaendelea kuona uhitaji uko wapi zaidi na tutaendelea kuchangia, lengo langu kuu ni kuona tunaenda kulibadilisha Jiji hili kwa kasi zaidi”-Dr. Tulia Ackson

Share To:

msumbanews

Post A Comment: