KITETO MANYARA 
Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara Bwana Tumaini Magesa amewataka wafugaji na wakulima katika vijiji vinavyounda ushirika wao wa kutunza rasilimali ardhi kwa ajili ya malisho ya Mifugo unaofahamika kama OLENGAPA kuheshimu taratibu za hati miliki za kimila na usajili wa ushirika huo  kwa mujibu wa sheria kwa faida ya kizazi cha leo na kesho.
Ametoa rai hiyo katika kijiji cha ENGANG’ONGARE alipokuwa akikabidhi hati miliki za kimila 9 na vyeti vitatu vya usajili wa Ushirika wa wafugaji wa kuendeleza nyanda za Malisho, katika mpango wa kimataifa wa kuendeleza maeneo yaliyohifadhiwa  kwa kutumia taratibu za kiasili au kimila na kutekelezwa na Jumuiko la Mali Asili Tanzania (TNRF) na  muunganiko  wa vijiji vya jamii ya kifugaji.( KINNAPA); kwa ushirikiano wa wizara ya mifugo na halmashauri hiyo;chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa(UNDP)na Umoja wa Ulaya (EU).
Bwana Magesa amesema kuwa kuwepo na matumizi bora ya ardhi ambayo  yamepangwa na kujulikana kisheria; itawezesha  kuondoa changamoto ya migogoro ya ardhi, iliyokuwa ikijitokeza wilayani humo, miaka iliyopita; na pia kwa faida ya kizazi cha leo na kesho.
Share To:

Post A Comment: