Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalla na mkuu wa mafunzo ya mgambo Kilolo wakiimba WIMBO wa Taifa 
Katibu tawala wilaya ya Kilolo Mwajuma Abass kushoto na kamati ya usalama wakiimba WIMBO wa Taifa 
Askari wa jeshi la akiba wakiimba WIMBO wa Taifa 
Askari wakionyesha uwezo wao wa singe
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ,mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdallah akifunga mafunzo ya jeshi la akiba kata ya Image 
Asia akiwapongeza wahitimu 
Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdallah wa nne kulia akiwa na katibu tawala Mwajuma Abasi mwente Kofi jeusi na wajumbe wa kamati ya usalama wilaya wakipiga picha ya pamoja na wahitimu wa mafunzo ya jeshi la akiba 

Serikali wilaya ya Kilolo mkoa wa Iringa imewataka vijana waliohitimu mafunzo ya jeshi la akiba (Mgambo)kata ya Image kuwa wazalendo na kufanya kazi za uzalishaji mali badala ya kutumia mafunzo hayo kupiga raia .


Rai hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Asia Abdallah leo wakati akifunga mafunzo ya mgambo hao kuwa ni vizuri wahitimu hao kwenda mitaani kuwakamata watuhumiwa wote wanaojihusisha na vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo ubakaji na mimba za wanafunzi .


Kuwa ndani ya wilaya ya Kilolo hataki kusikia wala kuona matukio ya unyanyasaji wa kijinsia wa aina yoyote ile na hategemei kusikia kuna mwanamke anayemfanyia vitendo vya kikatili mume wake.


Asia alisema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajenga vijana kuwa na uzalendo katika nchi yao na kupitia mafunzo hayo yataongeza   amani na utulivu ndani ya wilaya na mkoa wa Iringa .


"Leo mmekula kiapo cha kumtii Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amiri jeshi mkuu Rais wetu Dkt John Magufuli sasa sio leo mmekula kiapo kesho nisikie ninyi wenyewe mhusika na matukio ya uhalifu na unyanyasaji wa wananchi sitawavumilia nitawawajibisha nataka mkawe watii kwa kufanya kazi yenu kwa weledi " alisema Asia


Kuwa zimekuwepo tabia baadhi ya maeneo nje ya mkoa wa Iringa kusikia askari wakinyanyasa wananchi kwa kutumia Nguvu nyingi pindi wanaokwenda kuwakamata jambo ndani ya wilaya ya Kilolo hataki kusikia .


Alisema askari hao wa akiba wasikubali kutumika vibaya na wenyeviti wa vijiji  ,maafisa watendaji hata kama atakuwa yeye mwenyewe akitaka kuwatumia kunyanyasa wananchi wasikubali kufanya hivyo bali watumie weledi wao .


Asia alisema ndani ya wilaya ya Kilolo amepiga marufuku vijana kushinda vijiweni muda wa kazi  na wanawake wenye watoto na wajawazito kwenda katika vilabu vya pombe hivyo kazi moja wapo ya askari hao ni kusimamia sheria na maagizo mbali mbali ya serikali wakiwemo hayo ya vijana na wanawake wenye watoto kwenda .


Katika hatua nyingine mkuu huyo wa wilaya aliwataka vijana hao zaidi ya 90 waliopata mafunzo kutumia mafunzo hayo kuanzisha kikundi cha uzalishaji mali kama kwenda kulima  vibarua kwa umoja ili kupata mtaji wa kuendesha shughuli yao binafsi ikiwemo ya kilimo ambapo ofisi yake tawapa mbegu.


Pia alisema hajazuia wananchi wa Kilolo Kunywa pombe wakati wa kazi ila amezuia vilabu vya pombe kufunguliwa muda wa kazi na wananchi wanaokunywa pombe ruksa kunywa pombe wakati wowote ila wakiwa wanafanya kazi shambani

Share To:

Francis Godwin Mzee wa matukiodaima

Post A Comment: