Timu za Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Ofisi ya Rais Ikulu zimetinga hatua ya fainali ya michuano ya Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 ambayo inafanyika Aprili 28, 2024 jijini Arusha.

Mchezo huo umechezwa Aprili 28, 2024 katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha ambapo michezo ya Michezo ya Mei Mosi Taifa inaendelea kupamba moto na kuwapa burudani wakazi wa jiji hilo na viunga vyake.

Timu ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ndiyo imekuwa ya kwanza kutinga hatua ya fainali ya michuano hiyo kwa kuwafunga wapinzani wao timu ya Wizara ya Afya kwa jumla ya magoli 58 – 22 na kufuatiwa na timu ya Ofisi ya Rais Ikulu ambayo imewafunga timu ya Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi kwa magoli 38 - 31.

Bingwa wa mchezo huo anatarajiwa kukabidhiwa kombe wakati wa maadhimisho ya Siku Kuu ya Wafanyakazi Duniani ambayo kitaifa itafanyika jijini Arusha na Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Share To:

Post A Comment: