Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Bodi ya Nyama nchini imepiga marufuku matumizi ya magari yenye kutu katika kubeba nyama kwani kutu ni hatari kwa afya ya binadamu hivyo amesema kuwa serikali haitasita kuchukua hatua kali kwa watakaokahidi agizo hilo.

Akizungumza katika Maonyesho ya Teknolojia za Uchakataji wa nyama yaliyohudhuriwa na  Wanachama wa Chama cha Wachinjaji  na Wafanyabiashara wa nyama jijini Arusha ,Kaimu Msajili wa Bodi ya nyama Tanzania Imani Sichalwe amesema kuwa wamechukua hatua hiyo ili kulinda ubora wa nyama na kulinda afya za walaji  kwa kiuhakikisha kuwa magari yenye kutu hayataruhusiwa kubeba nyama pamoja na ubebaji wa nyama mgongoni.

Mwenyekiti wa Chama cha Wachinjaji Alex Lasiki ameiomba serikali isogeze mbele katazo la kutumia vigogo vya miti kukata nyama na kuweka mashine za kukata nyama kwani wachinjaji wengi wanakabiliwa na changamoto ya mitaji midogo ili waweze kujipanga kununua mashine za kisasa.

Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Ismail kulanga amesema kuwa jiji la Arusha litashirikiana na machinjio ya Arusha  Meat ili kuboresha mazingira ya machinjio hayo na kuhakikisha huduma bora zinatolewa.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: