NA HERI SHAABAN
TAASISI  ya Fahali Tuamke Maendeleo yasaisaidia Halmashauri ya Ilala kutatua changamoto za kijamii.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Fahari Tuamke Maendeleo Neema Mchau wakati wa mafali ya kumi na mbili shule ya Msingi Bangulo kata ya Gongolamboto  Wilayani Ilala.

Neema alisema taasisi ya Fahari Tuamke Maendeleo inashughulika na masuala ya Kijamii kwa ajili ya kuisaidia serikali hususani halmashauri ya Ilala     .

"Taasisi ya Fahari Tuamke maendeleo imekuwa karibu katika masuala ya kijamii katika shughuli mbalimbali ndani ya kata ya Gongolamboto na shule ya msingi Bangulo" alisema Neema.

Neema alisema mwaka huu Taasisi ya Fahari itamalizia ujenzi wa chumba cha darasa la Shule ya Msingi Bangulo ili watoto waweze kusoma katika juhudi za kuleta Maendeleo na kusaidia mpango wa Serikali ya awamu ya tano wa elimu bure na kukuza sekta uchumi wa viwanda.

"Katika Wilaya ya Ilala fahari Tuamke Maendeleo  tumejipanga katika kukuza viwanda vidovigo na kuendeleza viwanda vilivyopo kwa ajili ya kusaidia serikali ya Rais John Magufuli" alisema

Aliwapongeza waitimu wa darasa la saba wa shule hiyo na kuwataka wajiendelieze kielimu ili waweze kuwa viongozi wa baadae .

Katika mahafali hayo ya 12 mgeni rasmi Neema alinzindua harambee na kuwataka wadau wa elimu kushirikiana na serikali katika mpango wa elimu bure.


Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Wilfredi Luyagaza alielezea mafanikio ya shuĺe yake katika taaluma kwa kufaulisha watoto mwaka hadi mwaka.

Mwalimu Luyagaza alisema kwa kipindi cha miaka mitatu mwaka 2016 waitimu 141 waliofaulu 104 mwaka 2017 waitimu 161 waliofaulu 103 na mwaka 2018 waitimu 178 waliokwenda sekondari 138 ni sehemu ya kujivunia kwa ushirikiao wa wazazi na walimu.

Mwisho
Share To:

msumbanews

Post A Comment: