Taasisi ya ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Tanzania imeibuka mshindi wa kwanza Miongoni mwa Taasisi za Elimu kanda ya kaskazini. Ushindi huo ulitangazwa na Mgeni Rasmi wa sherehe za maadhimisho ya kilele cha maonesho ya Nanenane ya 26 kanda ya Kaskazini tarehe 8 Agosti 2019, Naibu Waziuri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mh. Abdalah Ulega.

 Akizungumzia ushindi huu Makamu Mkuu wa Taasisi, Prof Emmanuel J. Luoga,  amebainisha kuwa,  Ushindi huo ni motisha na hatua muhimu kwa taasisi hasa katika kufanya tafiti na ugunduzi ili kutatua changamoto za Viwanda na Jamii.

Aliongeza kuwa wakati wa maandalizi ya kushiriki kwenye maadhimisho haya, taasisi ilijikita zaidi kwenye maeneo ambayo yalikuwa ni vipaumbele vya maonesho ambayo yalikuwa Kilimo, Mifugo na Uvuvi hasa kwa lengo la kuleta sulkuhisho la matatizo yanayo ikumba jamii ya wafugaji na wakulima hapan nchini.

Prof. Luoga amesema tafiti zilizokuwa sehemu ya maonesho ya Taasisi ni pamoja na:

1. Matokeo ya utafiti juu ya Namna ya kuboresha uzalishaji wa migomba inayostahimili ugonjwa wa mnyauko.

 2. Matokeo ya utafiti juu ya njia ya kibaiolojia ya kudhibiti magugu vamizi katika malisho ya wanyama na mashambani. Utafiti huu unafanyikia katika hifadhi ya Ngorongoro.

3. Utafit juu ya Madawa asilia yanayoweza kutumika katika kuchakata ngozi/ kuiongezea thamani kwa matumizi mbalimbali kama kutengenezea viatu, mikoba ya akina dada na bidhaa nyinginezo.

4. Utafiti juu ya teknolojia ya kuondoa Magadi/Chumvi kwenye maji kwa matumizi salama nyumbani na viwandani.

5. Utafiti juu ya mfumo wa Tehama wa kujifunzia kwa watoto wadogo

Pamoja na hayo Taasisi ilikuwa ikiendesha mafunzo mbalimbali kwa wakulima,  Wafugaji na wadau mbalimbali ikiwemo mafunzo juu ya:

1. Njia bora za kuongeza thamani ya zao la ngozi katika mfumo mzima wa kuongeza thamani.

2. Matumizi mbalimbali ya Aloe hapa Tanzania ikiwemo faida na hasara za aina mbalimbali za Aloe.

3. Njia bora za kuzuia magonjwa ya Mlipuko baina ya binadamu na wanyama pamoja na mazingira kwa Afya moja (One Health)

4. Uhifadhi wa bayoanuai kwa afya yetu na uchumi wa nchi.

5. Mambo ya kuzingatia wakati wa uandaaji wa uji lishe kwa mtoto mwenye umri wa miezi 6 hadi 24.

Siku ya Sherehe za kilele cha maonesho,  tarehe 8 Agosti, timu ya wanawake wanasayasi waliweka vituo sehemu mbalimbali za viwanja vya maonesho na kutoa mafunzo mbalimbali yanayotokana na tafiti wanazozifanya.

Njia hii inawawezesha kufikisha ujumbe kwa walengwa papo kwa papo  lengo ikiwa ni kuhamasisha wanawake wengi kujiunga na fani ya sayansi na teknolojia na kuwawezesha watu wengi kupata maarifa yatakayo wasaidia kukabiliana na mazingira yanayowazunguka ili kuboresha hali yao ya kimaisha na kipato kwa ujumla.

Hayo yametamkwa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mh. Abdalah Ulega (MB) katika sherehe za kuhitimisha maadhimisho ya maonesho ya 26 ya Nanenane Kanda ya Kaskazini ambayo huhusisha mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara.

Wakati wa hotuba yake, Mh. Naibuwaziri aliipongeza Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela kama ifuatavyo
“Napongeza Juhudi kuwa za Wadau hawa waliofanikishautoaji wa wa elimu kwa wakulima, Wavuvi nan a Wafugaji. Naona sasa lengo la serikali la kupeleka nchi  kwenye uchumi wa kati” Alieleza Naibu Waziri wa KLilimo, Mifugo na Uvuvi, Mh. Abdalah Ulega
Share To:

msumbanews

Post A Comment: