Profesa Lazaro Busagala ni Mkurugenzi Mkuu wa TAEC nchini akizungumza na washiriki wa wa mafunzo ya namna ya kujikinga na mionzi wakati wa ukaguzi wa mizigo kwa kutumia mashine ya X-Ray.Picha zote na habari na Vero Ignatus.
Dkt.Remugius Kawala mtafiti mwanadamizi  na Mratibu wa tafiti wa mafunzo ya TAEC.

Washiriki wa Mafunzo yaliyoendeshwa na TAEC kuhusiana namna ya kuepuka madhara yatokanayo mionzi wakati wa ukaguzi wa mizigo,Watumishi 8 kutoka TRA na mmoja kutoka katika hoteli ya 4point by Sheratoni iliyopo jijini Arusha(New Arusha Hotel )
Mkurugenzi Mkuu wa TAEC Nchini Profesa  Lazaro Busagala akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi 8 kutoka TRA na mmoja kutoka katika hoteli ya 4point by Sheratoni iliyopo jijini Arusha(New Arusha Hotel )mara baada ya kumalizika kwa mafunzo ya siku tano ya namna ya kuepuka madhara yatokanayo mionzi wakati wa ukaguzi wa mizigo,

Washiriki wa Mafunzo yaliyoendeshwa na TAEC kuhusiana namna ya kuepuka madhara yatokanayo mionzi wakati wa ukaguzi wa mizigo,Watumishi 8kutoka TRA na mmoja kutoka katika hoteli ya 4point by Sheratoni iliyopo jijini Arusha(New Arusha Hotel )katikati ni mwanadada pekee aliyeshiriki katika mafunzo hayo Devotha Mwenda kutoka TRA Makao makuu Dar es salaam.

Mkurugenzi mkuu wa TAEC Nchini Profesa Busagala akimkabidhi cheti cha mafunzo hayo Afisa Usalama Mwandamizi Idara ya mambo ya ndani TRA kutoka makao makuu Jijini  Dar es salaam
Mmoja wa washiriki wa Mafunzo hayo kutoka TRA Majid Lema akipokea cheti cha mafunzo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TAEC nchini Profesa Lazaro Busagala.

Albert Mwangila Afisa mkuu wa Idara ya mambo ya ndani kutoka TRA makao makuu Dar es salaam akitoa neno la shukrani mara baada ya mafunzo hayo kukamilika.

Na.Vero Ignatus,Arusha.

Tume ya Nguvu za Atomiki Nchini imeendesha mafunzo ya siku tano kwa watumishi wa Mamlaka ya Mapato nchini lengo likiwa ni kujua namna ya kujilinda na mionzi wakati wa ukaguzi wa mizigo ,kwa kutumi a mashine za X-RAY .

 Profesa Lazaro Busagala ni Mkurugenzi Mkuu wa TAEC nchini,amesema lengo la nguvu za Atomiki Tanzania ni kuendesha mafunzo ya aina hiyo mara kwa mara, kwani ni muhimu ili kuweza kuhakikisha kwamba wananchi kwa ujumla wao wanakuwa salama kutokana na madhara yanayoweza kujitokeza kwasababu ya mionzi  au Teknolojia ya Nyuklia 

Profesa Busagala amesema kuwa hata katika viwango vya Kimataifa ,Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani International Atomic Energy Agency ( IAEA) linatumia kuwa ni kigezo kimoja wapo kuiweka nchi katika kundi la kuwa  salama ikiwa kuuna mafunzo ,amesema kama hakuna mafunzo ni kwamba watu hawana uelewa wa kutosha na mambo yanakwenda bora yaende na watu wanatumia visivyo.

“Kwasababuhiyo pia tunabadilisha kanuni zinazowalinda wananchi kutokana na madhara ya mionzi tayari katika hatua za ndani ya Tume ya nguvu za Atomiki nchini Tanzania tumeshapitisha na tumeshapeleka kwa serikalini,na serikali sasa inaendelea kutumia kwa muda kuzipitia na mwanasheria mkuu wa serikali anazipitia,na zikishwa pitishwa tuweze kuweka mambo vizuri zaidi “Alisema Profesa.

Dkt.Remugius Kawala ni mtafiti mwanadamizi  na mratibu wa tafiti wa mafunzo ya TAEC amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuongeza uelewa kwa wale wanaoratibu mashine hizo,pamoja na uelewa wa jamii,na kuripoti namna ya watu wanaokwenda mipakani na Bandarini kutumia hizo mashine na kuwasaidia wadhibiti kuwa na watu ambao wanauelewa wakutumia hizo mashine.

“Mzigo unapoingia nchini kwa mara ya kwanza lazima ukaguliwe kwa mashine,kwahiyo ukiangalia tunamaeneo mengi sana ya hizo check point,bandari,mamlaka mbalimbali nchini,viwanja vya ndege,mahoteli makubwa,ila kwa sasa tumeanza na Mamlaka ya Mapato nchini TRA na baadae tutaendelea na Mamlaka nyingine Nchini”Alisema Dkt.Kawala.

Dkt Kawala amesema kuwa wanashauri  wakati mashine ya Scan ikiwa haijazimwa hawaruhusu  mtu kuingiza  mkono kwani mionzi inayotoka katika mashine hiyo  husababisha baadhi ya seli za mwili kufa japo kuwa hawajui ni kwa kiwango gani kwa wakati huo ,amesema  ikiwa inajirudia mara kwa mara kuna  uwezekano wa  kusababisha madhara  mengine kama ya kansa.

“Mashine ikishamulika ule mzigo unatakiwa uache utoke kabisa kwenye mkanda uje uupokelee nje kabisa hata Yule operetta ukimuangalia kwa umakini utaona hawai kukimbilia lile begi,kwasababu kunavidhibiti vinaitwa leedsheets”alisema Dkt.Kawala.

 Albert Mwangila ni Afisa mkuu wa Idara ya mambo ya ndani kutoka TRA makao makuu Dar es salaam amesema kuwa mafunzo yalikuwa yakilenga namna ya kutumia mashine bila ya kuleta madhara kwa mtumiaji ,wakati huohuo kuweza kuwalinda wateja pamoja nawageniwanaotembelea ofisi za Mamlaka hiyo .

“ Mashine hizo  tulizopatiwa elimu ni kwaajili ya ukaguzi,mashine zinazotoa mionzi ambazo ni  X-Ray,na mashine ya kuskani mizigo “Alisema Mwangila.

amesema kuwa wanaishukuru TAEC kwa kuwapatia mafunzo hayo sambamba na mambo mengi ambayo Taasisi hiyo imeyafanya kwaajili yao wakati wa mafunzo,wamekuwa na wataalam tofauti kwa nyakati mbalimbali na wote walikuwa wamebobea katika maeneo yao.

Hata hivyo mafunzo hayo yamefungwa leo huku idadi ya wahitimu wakiwa ni watumishi nane kutoka mamlaka ya mapato nchini TRA , na mmoja M
eneja usalama kutoka katika hoteli ya 4point by Sheratoni iliyopo jijini Arusha(New Arusha Hotel )

Mwisho.
Share To:

Vukatz Blog

Post A Comment: