Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Arusha akikabidhiana mkataba na kiongozi wa kampuni ya SINOHYDRO CONSTRUCTION LTD kutoka nchini China.
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Dkt. Maulid Suleimani Madeni akisaini mkataba mdogo(Addendum) wa ujenzi wa barabara ya Kisongo bypass
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Mhe. Kalisti Lazaro akiweka sahihi katika mkataba mdogo(Addendum) wa ujenzi wa barabara hiyo ya Kisongo bypass

Halmashauri ya Jiji la Arusha imesaini mkataba mdogo wa Addendum na kampuni ya SINOHYDRO CONSTRUCTION LTD kutoka China ikiwa ni kazi ya nyongeza ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Kisongo bypass hadi Olasiti yenye urefu wa kilomita 3.442 itakayo gharimu fedha za kitanzania shilingi bilioni 4.1

Ujenzi wa barabara hiyo ya Kisongo upo chini ya mradi wa TANZANIA STRATEGIC CITIES PROJECT (TSCP)-AF2 ambapo unahitajika kukamilika ndani ya miezi minne kuanzia 11 Septemba 2019 hadi 11 Januari 2020.

Akizungumza wakati wa utiaji wa saini hiyo Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dkt. Maulid Suleimani Madeni amemsisitiza mkandarasi wa miradi huo kufanya kazi kwa ubora na kwa muda uliopangwa ili mradi huo ukawe faida kwa wananchi wa maeneo hayo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: