
kaimu mkurugenzi wa mwendeshaji wa kituo hicho cha mikutano Victor Kamagenge akizungumza na waandishi
Na Woinde Shizza , Arusha
Wafanyakazi wa kituo cha mikutano cha Arusha(AICC) kwakushirikiana na wafanyakazi wa baraza la utunzaji na usimamizi wa mazingira leo
wamehitimisha kilele cha Wiki ya utumishi Umma kwa kufanya usafi
katika baadhi ya maeneo ya jiji la Arusha ikiwepo hospital ya AICC
inayomilikiwa na kituo .
Akiongea
na waandishi wa habari kaimu mkurugenzi wa mwendeshaji wa kituo hicho
cha mikutano Victor Kamagenge alisema kuwa katika wiki hii ya
kuazimisha wiki ya watumishi wa umma wao kama kituo wamefanya kazi
mbalimbali ikiwemo uongozi wa kituo kukutana na wateja wao waliopanga
katika ofisi zao pamoja na Nyumba zao, wafanyakazi wa kituo hicho na
wamehitimisha leo kwakufanya usafi katika hospital hiyo inaomilikiwa na
kituo.
Alisema kuwa
lengo la kuazimisha siku hii kwakufanya usafi katika hospital hii ni
kusaidia kuweka mazingira mazuri ya hali ya usafi katika hospital yao
ambayo pia ni moja ya sehemu inayoingizia mapato kituo
"mnajua
tumeona tuje kufanya usafi hapa hospital ili mazingira yetu yazidi kuwa
rafiki kwa wateja wanaokuja hapa kupata huduma, haiwezekani mgojwa
anakuja hapa kutibiwa akimaliza anaondoka na ugonjwa mungine kutokana na
mazingira kuwa machafu hivyo ndio maana tumekuja kufanya usafi "alisema
Kamagenge
Alibainisha
iwapo mazingira yatakuwa masafi na salama pamoja na huduma kuwa nzuri
itasaidia ata wateja kuja kwa wingi na watapata fedha itakao saidia ata
kupata gawiwo la serikali.
Naye
meneja baraza la utunzaji na usimamizi wa mazingira (NEMC)kanda ya
kaskazini Lewis Nzari Alisema kuwa wao kama wasimamizi wamazingira
wameamua kujiunga pamoja na kituo hichi kufanya usafi katika maeneo ya
jamii kwani wanatambua kuwa mazingira yakiwa safi yanachangia
kuhakikisha afya za watu zinakuwa nzuri.
Aidha
pia aliwapongeza wananchi wa mkoa wa Arusha na kanda ya kaskazini kwa
ujumla kwa namna walivyopokea katazo la waziri mkuu Kasimu Majaliwa la
kuacha kutumia Mifuko ya plastiki ,kwani wananchi wamepokea kwa
muitikio mkubwa.
"mazara
ya matumizi ya Mifuko ya plastick ni mengi sana kama vile uchafuzi wa
mazingira, pia Mifuko hii inasababisha magonjwa mengi kama vile kansa
na magonjwa ya uzazi "alisema Nzari
Alitoa
wito kwa wananchi kuendelea kupiga Vita matumizi haya ya Mifuko ya
plasticki kwa kuwapa elimu wananchi wote ambao wanatumia pamoja na
kuwakataza kutumia, maathimisho haya ya juma la utumishi wa uma
yanafanyika kila mwaka na kauli mbiu ikiwa ni "kujenga Utamaduni wa
utawala na matumizi ya tehama na ubunifu katika utoaji wa huduma
jumuishi".
Picha baadhi ya wafanyakazi wa NEMC na AICC wakifanya usafi katika hospital ya AICC
Post A Comment: