Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Jacob Mtalitinya (Kushoto)
akipokea "T-Shirt" ya mashindano kutoka kwa Afisa utamaduni wa manispaa
hiyo Kiheka Charles (kulia
Kikundi cha Wasafi Dancers wakitoa burudani wakati wa mashindano ya "Sumbawanga Talent Search"
Kikundi cha Swax Boys Dancers wakitoa burudani wakati wa mashindano ya "Sumbawanga Talent Search"
Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Jacob Mtalitinya
amewasihi vijana wa Manispaa ya Sumbawanga kujitokeza kwa wingi katika shindano
la kutafuta vipaji ili kuitumia fursa hiyo katika kuviibua na kuviendeleza vipaji
vyao huku wakiitangaza Manispaa pamoja na Mkoa wa Rukwa kwa ujumla.
Kikundi cha Wasafi Dancers wakitoa burudani wakati wa mashindano ya "Sumbawanga Talent Search"
Kikundi cha Swax Boys Dancers wakitoa burudani wakati wa mashindano ya "Sumbawanga Talent Search"
Mmoja wa Wasanii wa Sumbawanga akitoa burudani katika mashindano ya "Sumbawanga Talent Search" |
Amesema kuwa kwa muda mrefu Mkoa wa Rukwa hasa wilaya
ya Sumbawanga imekuwa na sifa ambayo wengi wakiisikia wanakuwa wanatishika
hivyo shindano hili ni fursa ya kuonyesha mambo mazuri yanayopatikana ndani ya mji
wa Sumbawanga na Mkoa. Ametoa wito kwa wananchi, vijana, pamoja na wazazi kujitokeza
na kuwarusu vijana wao kuonyesha vipaji vyao kuvitumia na kuhakikisha
wanajiimarisha siku zijazo kujipatia ajira.
“Idara ya maendeleo ya Jamii kwa kushirikiana na Afisa
utamaduni tumeona tuwe na hili shindano ambalo litatumika kuibua vipaji lakini
pia kuwaendeleza vijana ambao tunaaamini wakiendelezwa watatengeneza ajira, kwahiyo
kipaji ni ajira, hivuyo niwasihi sana vijana wa Sumbawanga kutumia nafasi hii
kuhakikisha kwamba wanaendeleza vipaji vyao,” Alisisitiza.
Kwa upande wake Afisa Utamaduni wa Manispaa ya
Sumbawanga, Kiheka Charles amesema kuwa manispaa ya Sumbawanga ina vipaji vingi
na nia ya kuanzisha mashindano hayo ni kutoa muongozo kwa wasanii wenye vipaji mbalimbali
kuweza kuyafikia malengo yao.
“Ofisi ya Mkurugenzi kupitia ofisi ya afisa utamaduni Manispaa
ya Sumbawanga tuliamua kuandaa shindano hili lenye lengo la kuwasaidia vijana
kuitangaza sanaa yao, kukuza vipaji vyao, na kuweza kuitumia sanaa kama chanzo
cha ajira na kunufaika, hivyo basi tunaomba wasanii mbalimbali wenye vipaji
wajitokeze kwa wingi kushiriki,”
Halikadhalika, baadhi ya wasanii waliohudhuria kwenye
mashindano hayo waliupongeza uongozi wa halmashauri kwa kuwathamini na kuwajali
na kuomuomba aendelee kuwaibulia vitu vingine ambavyo vitakuwa ni fursa kwa
vijana ili kuweza kuitangaza sumbawanga na Mkoa.
Mmoja wa washiriki wa mashindano hayo Switbert Filbert
a.k.a Fire Music alisema “Tunamshukuru sana Mkurugenzi kwa kuanzisha shindano kama
hili na tunamuomba kama kuna vingine anavifikiria avifanye kwasababu mkoa wa
rukwa upo nyuma katika sanaa, michezo na mengine hivyo tunawaahidi watanzania,
wanarukwa na Sumbawanga kuwa tutafanya vizuri.”
Aidha, mshiriki mwenzie wa mashindano hayo Daniel
Benedicto a.k.a Dabeto alisema “ mashindano haya yakiendelea kwa Mkoa wetu wa
Rukwa sana sana Sumbawanga tunaweza tukatoka sana kwasababu wasanii wengi
hawapati muda wa kuonyesha vitu vyao wazi kama vile kupata fursa ya “ku-perform”
mbele za watu, wengi tulikuwa tunahofu kwamba unaweza kuonyesha sehemu gani,
wengi walikuwa wanjificha ndani, hii ni fursa ya kutengeneza mashabiki.”
Mashindano hayo ya “Sumbawanga Talent Search” yenye
kauli mbiu “Kipaji ni Zawadi Thamini Sanaa Yako” yanasimamiwa na Afisa
utamaduni ambaye pia ni msanii wa “Hip-Hop” aliyedhamiria kushirikiana na
Mkurugenzi wa manispaa hiyo kuinua vipaji vya vijana wa Sumbawanga.
Post A Comment: