Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Ndugu Patrobas Katambi ametoa pongezi zake kwa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) kwa kuanzisha Ofisi ndogo jijini humo na kuwapa mbinu ya kuboresha sekta ya Utalii.
DC Katambi amesema kitendo cha TANAPA kufungua Ofisi yao jijini humo kutaongeza hadhi ya Dodoma kuwa Makao Makuu kwani kutaondoa usumbufu wa wananchi waliokua wakihitaji huduma za kitalii kusafiri kuzifuata Dar es Salaam na Arusha.
DC Katambi ameyasema hayo wakati alipokua akizindua warsha ya wanahabari kupata taarifa ya uanzishwaji wa Ofisi za TANAPA Dodoma ambapo ndipo yalipo Makao Makuu ya Nchi pamoja na taarifa zingine za uhifadhi na utalii.
"Jambo mlilolifanya leo mnapaswa kupongezwa, pamoja na kwamba Dodoma hatuna mbuga za wanyama lakini kitendo cha kufungua Ofisi zenu hapa kumeongeza hadhi ya Makao Makuu na itatuongezea pato kubwa, pia mtarahisha huduma zenu kwa mikoa ya kanda ya kati ambayo ilikua ikiteseka kuzifuata huduma zenu Dar es Salaam au Arusha yalipo Makao Makuu yenu.
" Niwapongeze pia kwa kuandaa hii ya warsha kwa wanahabari, watumieni vizuri hawa ndugu zetu katika kuzitengeza hifadhi zetu ambazo kwa hakika zimebarikiwa kuliko nyingine zote duniani, kama mtawaongezea maarifa wandishi kwa kuwapeleka kwenye hifadhi kujifunza kwa vitendo zaidi kutawaongezwa ufanisi mkubwa katika kuandika habari za Tanapa na utalii kwa ujumla. Wandishi ndio watu wanaojua lugha sahihi ya kuandika ili watanzania wavuvutiwe kutembelea vivutio vyetu, shirikianeni nao ili kukuza sekta yetu ya utalii," amesema DC Katambi.
Aidha ametoa wito kwa watanzania kutembelea mbuga za wanyama ili wawe mabalozi wazuri katika kuisemea Nchi yao na kuwataka Tanapa kurudisha mashindanano kwa wandishi wa habari katika kuripoti na kutangaza habari za Tanapa jambo ambalo anaamini litachochea maendeleo ya sekta ya utalii nchini.
Imetolewa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Dodoma.
Post A Comment: