Mwenyekiti
wa TLP, Augustino Mrema amemtaka waziri wa mambo ndani, Kangi Lugola
kuwachukulia hatua wabunge wanaomchafua Rais John Magufuli.
Amesema
kuna vikundi vya wabunge ambao wanatengeneza chokochoko dhidi ya Rais
na kwamba hatua zichukuliwe kabla hawajatimiza azma yao mbaya dhidi
yake.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana Agosti 3 katika ofisi za chama hicho
zilizopo Magomeni, Dar es Salaam, Mrema amesema wabunge hao ambao baadhi
ni wanachama wa CCM wanahatarisha usalama wa Rais kwa kumchonganisha na wananchi.
Mrema
ambaye alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani katika serikali ya awamu ya
pili amesema anawafahamu wabunge hao licha ya kutowataja majina yao.
Ameahidi kumpa ushirikiano Waziri Lugola endapo atahitaji kwa kuwa anafahamu mambo hayo kiundani.
"Mimi
nimewasikiliza wabunge tena wa CCM kwa mfano waliosema Rais amechukua
Trilioni 1.5 ni kweli au ni kumchafua? Kwa hiyo kuna hiyo tabia imezuka
ya kumzulia Rais maneno ya uongo na ya kumdhoofisha,"alisema.
Alisema vikundi hivyo nimekuwa vikitengeneza "chokochoko" ambazo zinalenga kumchonganisha Rais na wananchi.
"Wabunge hao nawafahamu na niko tayari kuwataja kabla hawajatimiza uovu kama ilivyokuwa kwangu,"amesema.
Alieleza kuwa atakuwa mstari wa mbele kuhakikisha Rais anaheshimiwa na kuungwa mkono kwa sababu kazi aliyonayo ni kubwa.
Pia
amemshauri Rais Magufuli kuwa makini na viongozi wake kwa kuwa wengi
wanafanya mambo kwa kutafuta ‘kiki’ na huenda wakawa si rafiki katika
kazi zake.
Post A Comment: