Yanga itaondoka leo ikipitia Dubai kuwavaa USM Alger katika mechi ya mkondo wa kwanza itakayopigwa Jumapili ya wiki hii mjini Algiers.
Meneja wa timu hiyo, Hafidh Saleh amesema kuwa kikosi kipo tayari na wamejikamilisha kimaandalizi kwa ajili ya safari hiyo.
Mbali na maandalizi, Saleh amekanusha uwepo wa taarifa zilizoeleza kuwa wachezaji wamegoma kuhusiana na madai ya stahiki zao ikiwemo mishahara.
Kauli hiyo imekuja kutokana na sintofahamu ya viongozi wa Yanga kushindwa kuonesha ushirikiano wa kueleza namna maandalizi yanavyoenda kuelekea safari hiyo huku kukiwa na tetesi kuwa wachezaji wamegoma wakidai mishahara.
Hata hivyo Saleh leo asubuhi amekanusha uwepo wa taarifa hizo huku akieleza kuwa haweze kuelezea kwa kina suala la wachezaji kugoma.
Post A Comment: