Mwanamuziki wa Bongo fleva Rose Kimario maarufu kama Rosa Ree ameingia Kwenye ulimwengu wa kibiashara baada ya kufungua mini supermarket yake mpya aliyoipa jina la Rosa Ree Mini Supermarket.

Risa Ree alitumia ukurasa wake wa Instagram kutangaza habari hiyo njema.

Rosa Ree amefanya Interview na Millard Ayo Tv na ameweka wazi kuwa imemgharimu zaidi ya milioni 30 kuwekeza Kwenye biashara ile

"Ile ni Supermarket yangu na ninategemea kuifungua rasmi wiki ijayo hivi sasa tupo Kwenye maandalizi ya mwisho ni kitu ambacho nilipanga kufanya kwa muda mrefu sasa.

"Kusema ukweli nimewekeza pesa nyingi lakini kwa haraka haraka nimewekeza zaidi ya milioni 30 na nina mpango wa kufungua supermarket kubwa zaidi ya ile”.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: