MSHAM-BULIAJI wa Simba, Mganda, Emmanuel Okwi amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo kwa kusema kuwa watahakikisha wanashinda mechi zote zilizobakia ikiwemo ya Singida United ili kutwaa ubingwa huku akisisitiza hawatajali wanahitaji pointi ngapi.
Simba inaongoza Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 65, mbele ya Azam FC inayoshika nafasi ya pili ikiwa na pointi 49 ikifuatiwa na Yanga yenye pointi 48.
Simba inahitaji pointi mbili kuweza kutangaza ubingwa huku ikiwa na mechi tatu mkononi kabla ya kumalizika kwa msimu huu.
Akizungumza na Championi Jumatano, Okwi alisema kuwa kwa upande wao wanachokiangalia wakati huu ni kuweza kushinda mechi zote zilizobaki bila ya kuangalia wanataka pointi ngapi.
“Sisi mpaka sasa hivi tunajua tuna mechi tatu, na hatuangalii pointi moja au mbili lakini kikubwa ni kwamba tunataka kushinda mechi zote, tutaendelea kupambana, tunaenda Singida kupamba na kuhakikisha tunapata ushindi ili kuweza kufikia malengo.
“Lakini namshukuru Mungu kwa kucheza mechi nyingi na kuniwezesha kufunga mabao lakini rekodi za watu haziwezi kunipa presha yoyote, nikifanikiwa kufunga katika mechi ijayo itakuwa vizuri zaidi kwa sababu kwetu kikubwa ni timu kushinda,” alisema Okwi ambaye anaongoza kwa kufunga mabao msimu huu akiwa na mabao 20
Post A Comment: