Ligi Kuu Spain inaendelea leo kwa Mabingwa watetezi wa taji hilo FC. Barcelona wakiwa wanakawaribisha Real Madrid kwenye Dimba la Cam Nou.
Barcelona wanashuka dimbani wakiwa tayari wameshanyakua ubingwa huo pamoja na Kombe la Mfalme huku wapinzani wao Madrid wakiwa hawajachukua ubingwa wowote msimu huu.
Kuelekea mechi hiyo maarufu kama El Clasico, Kocha wa Madrid, Zinedine Zidane, amesema kuwa itakuwa vigumu kuwapongeza Barcelona kabla ya mchezo kutokana na kuutwaa ubingwa ligi.
Zizou ameeleza hayo kutokana na Barcelona walishindwa kuwapa heshima yao Madrid baada ya kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia kwa ngazi ya klabu msimu uliopita.
Zidane amesema kuwa hadhani kama suala hilo litawezekana sababu kama wao wangeipa heshima Madrid, basi wasingeweza kuvunja utamaduni wa kupongezana kama ilivyozoeleka.
Mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu na wadu wengi wa soka duniani, itaanza majira ya saa 3 na dakika 45 usiku wa leo.
Post A Comment: