Mchekeshaji wa kike Bongo aliyejizolea umaarufu mpaka nje ya nchi Katarina Karatu, amesema kauli ya Ebitoke kwamba Tanzania hakuna wachekeshaji wa kike, amekosea kwani wako wengi sana.

Akizungumza na www.eatv.tv, Katarina amesema licha ya kwamba hajisikii kumuongelea Ebitoke, lakini kauli aliyoitoa haileti maana na inavunja moyo, kwani wachekeshaji wapo wengi isipokuwa mashabiki ndio wanaamua nani ni mkali zaidi.

“Yule ni mtu mzima anajua anachofanya kwa hiyo kuanza kumuongelea sijisikii kwanza, nahisi sifanyi kitu sahihi, kuhusu wachekeshaji wa kike kwanza anakosea, wapo wengi tu kuna watu wanafanya vizuri, ni mashabiki wanaamua nani ni bora na nani anavamia fani, ila kuhusu yeye sihitaji kumuongelea sana kwa sababu zangu binafsi”, amesema Katarina.

Mchekeshaji huyo ameendelea kwa kusema kwamba ili kuthibitisha kuwa wachekeshaji wazuri Tanzania wapo, hivi karibuni amepata mwaliko nchini Kenya ambapo atapanda jukwaa moja na wachekeshaji kutoka nchi nyingine za Afrika Mashariki, Anne Kansiime wa Uganda, Idirs Sultan wa Tanzania na wengine wa Kenya.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: