Na George Mganga

Kocha Msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa, amesema kuwa hakuwa na uhakika kama Mbeya City walizidi Uwanjani baada ya mchezaji mmoja kupewa kadi nyekundu.

Nsajigwa ameeleza hayo wakati akizungumza na Azam TV baada ya mchezo kati ya Mbeya City dhidi ya Yanga kumalizika Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Kocha huyo amesema kuwa hakuwa na uhakika kama Mbeya City walizidi, lakini aliona kama walikuwa 11 ilihali beki wao Ramadhan Malima alikuwa ameshapewa kadi nyekundu.

Aidha, Nsajigwa ameeleza kuwa wakati akimuuliza Kamisaa wa mchezo alikuwa amepandwa na munkari hivyo kujikuta akiona mambo yakiwa tofauti Uwanjani baada ya Kamisaa huyo kumwambia hawajazidi.

Nsajigwa alimuuliza Kamisa baada ya Mbeya City kufanya mabadiliko ya mchezaji mmoja na kumuingiza mwingine, kitu ambacho kilimchanganya na kuona hawako 10 Uwanjani na badala yake akawona wakiwa 11 kama mwanzo.

Mbali na yote hayo, Nsajigwa amewapongeza Mbeya City kwa kupambana na kurudisha bao wakiwa pungufu ambapo walipata bao hilo zikiwa zimesalia dakika 6 pekee mpira umalizike.

Mchezo huo wa ligi, ulimalizika kwa sare ya mabao 1-1 ambapo Yanga walifunga kupitia Rafael Daud, na City kupitia Iddy Naddo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: