Mfanyakazi wa Shirika la Umeme (Tanesco) Kibaha, Chande Kipae, amefariki dunia baada ya kunaswa na umeme wakati akiondoa nyaya za umeme zilizokuwa zimekatika.

Tukio hilo limetokea April 16 saa tisa jioni wakati Chande akiwa na mtoto wake Jumanne Chande wakielekea mjini kutafuta mahitaji ya familia.

Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi umethibitisha kupokea mwili wa marehemu huyo na kwamba waliufanyia uchunguzi na kukabidhi kwa ndugu kwa ajili ya taratibu za mazishi.

Taarifa kutoka Shirika la Umeme Tanesco Mkoani Pwani, Madulu zilithibitisha kutokea kwa kifo cha mfanyakazi huyo huku ikidaiwa kwamba siku ya tukio aliomba ruhusa ofisini kwa ajili ya masuala yake binafsi.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: