Blandina Chagula ‘Johari’
MUIGIZAJI mkongwe kwenye tasnia ya filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ ametoa kali ya mwaka baada kusema kuwa na yeye atakwenda kwenye Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda kudai kuwa ameachwa wala sio kutelekezewa mtoto au kunyimwa matunzo ya mtoto.
Akizungumza na Risasi Jumamosi Johari alisema, yeye hana shida ya kuachiwa mtoto bali ataenda kusema kuwa aliachwa na mtu ambaye alikuwa akimpenda hivyo aangalie utaratibu ambao na yeye atasaidiwa kama mwanamke aliyeachwa.
Post A Comment: