Dkt. Mwakyembe :Vijana wanatakiwa kutumia vizuri mitandao ya kijamii hususani kwenye upatikanaji elimu ya mambo mbalimbali.
Dkt.Mwakyembe:Vyombo vya habari vinatakiwa kutoa habari kwa kuzingatia maadili na sheria ya habari.
Dkt.Mwakyembe:Vyombo vya habari ni vya muhimu katika kumuwezesha Mtanzania kufahamu yanayoendelea katika nchi hususani katika kuelekea kwenye uchumi wa viwanda.
Dkt.Mwakyembe:Serikali inazingatia uhuru wa habari hasa katika mambo yanayojenga nchi kwa kuleta maendeleo.
Dkt.Mwakyembe: Serikali haitafumbia macho kwa chombo chochote cha habari kitakacho toa habari za uwongo na uchochezi.
Dkt.Mwakyembe: Serikali ipo tayari kupokea ukosoaji wowote utakao tolewa na vyombo vya habari ambao unajenga na kuleta maendeleo ya nchi.
Dkr.Mwakyembe: Amevitaka vyombo vya habari hasa redio kuwasaidia wasanii wachanga kukua katika tasnia ya muziki.
Dkt.Mwakyembe: Wananchi wa Arusha wanatakiwa wajifunze zaidi jinsi ya kuboresha ujasiliamali, na jinsi yakunufaika nao hasa katika sekta ya utalii.
Dkt.Mwakyembe: Arusha kuna fursa nyingi,wananchi wanatakiwa wanufaike nazo.
Imetolewa na:
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha
11/3/2018.
Post A Comment: