Mwanamitindo na Mjasiliamali Jokate Mwegelo ambaye pia ni Kaimu Katibu Hamasa wa Jumuiya ya Vijana wa CCM, ameibuka na kudai anatarajia kuolewa 'kuwa mke wa mtu siku za hivi karibuni' licha ya kumficha mwanaume ambaye atamuoa.
Jokate ametoa kauli hiyo mchana wa leo (Machi 20, 2018) kupitia ukurasa wake wa kijamii akiwa wahabarisha wadau wake wakae mkao wa kula kusherehekea tukio hilo ambalo amelipanga kulifanya katika siku za usoni.
"March Quen, karibu nitakuwa mke wa mtu fulani na mama watoto wake. 'God is great and faithful, grown but forever a baby girl'. Ni kwa neema tu na rehema zake Mungu. Thank you loves for dragging me out to take these", amesema Jokate. 
Jokate Mwegelo ameweza kuweka uwazi wa maisha yake ndani ya siku aliyoweza kuletwa duniani 'kuzaliwa' miaka kadhaa iliyopita tarehe na mwezi kama wa leo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: