Rais wa zamani wa Marekani, Barack Obama ameunga mkono maandamano yanayofanyika nchini humo yanayoshinikiza kuundwa kwa sera mpya juu ya umiliki silaha.
Rais Barack Obama alipozuru Dar es Salaam, Tanzania 2013
Barack Obama
Barack Obama na mkewe Michelle wameunga mkono maandamano hayo ambayo yalifanywa na wanafunzi siku ya jana kwenye viunga vya jiji la Washington.
Mimi na mke wangu tumehamasika na kushawishiwa na maandano ya leo (jumapili) yanayofanywa na wanafunzi nchi nzima. Endeleeni kutupigania, Hakuna jambo linaloshindikana kwenye sauti za mamilioni ya watu wanaohitaji mabadiliko,“ameandika Barack Obama kwenye ukurasa wake wa Twitter.
Miji mingine ambayo wananchi waliandamana ni Boston, New York, Chicago, Houston, Minneapolis, Phoenix, Los Angeles na Oakland, California, katika idadi ambayo ilionekana wakati wa enzi za Vita vya Vietnam, na kuwazoa wanaharakati ambao kwa muda mrefu wamevunjwa moyo na mkwamo katika mjadala wa umiliki wa silaha na kuzijumuisha sauti nyingi mpya za vijana.
Waandamanaji hao ambao waliongozwa na manusura wa shambulio la shule mjini Parkland, Florida ambalo liligharimu maisha ya watu 17 Februari 4.
Walimu, wanafunzi na viongozi wa Chama cha Democratic wamekuwa wakimshinikiza Rais Donald Trump kuunga mkono hoja ya mabadiliko ya sera za umiliki wa silaha za nchini humo.
Mwezi Februari mwaka huu wanafunzi wapatao 17 waliuawa kwa kushambuliwa kwa risasi na mwanafunzi mwenzao, tukio ambalo lilibua hisia kali kwa wananchi nchini humo wengi wakitaka sera ya umiliki wa silaha nchini humo ibadilishwe.
Hata hivyo, Rais Trump bado ameonekana kufumbia macho mchakato mabadiliko ya sera za umiliki wa silaha ambapo hadi sasa hajatoa tamko lolote juu sakata hilo.
Kwa upande mwingine, Chama cha wamiliki wa bunduki nchini Marekani (NRA) kinachoelezwa kuwa ni moja ya makundi yenye ushawishi mkubwa zaidi katika bunge la Marekani kimethibitisha  kuwa tangu kuanze kwa maandamano hayo wikiendi iliyopita mauzo ya silaha yameporomoka .
Mwaka 2016, NRA walitumia jumla ya dola milioni $4 kupata uungwa mkono wa wanasiasa juu ya kupinga mabadiliko ya sera umiliki wa silaha.
Imeelezwa kuwa NRA walitumia zaidi ya dola milioni $50 katika kampeni za Rais Donald Trump kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2016.
Kwenye kampeni za uchaguzi huo Rais Trump alijinadi kuwa haoni tatizo kuruhusu kila Mmarekani kumiliki silaha kwani watu wanaotekeleza mauaji ni magaidi sio Wamarekani wema.
Sheria ya umiliki wa silaha nchini Marekani ni kwa watu wote waliofikisha miaka 18 na kuna baadhi ya majimbo kama  Alaska, Minnesota na New York mtu yeyote kuanzia miaka 16 anaweza kuuziwa bunduki hata bila ya usimamizi wa wazazi wake.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: