Waamuzi wanne wa Tanzania wameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Africa(CAF) kuchezesha mchezo wa kombe la Shirikisho kati ya Fosa Juniors ya Madagascar na As Port Louis ya Mauritius utakaochezwa Machi 18,2018 Madagascar.
Waamuzi walioteuliwa ni mwamuzi wa kati kati Elly Ally Sassii atakayesaidiana na Ferdinand Chacha mwamuzi msaidizi namba moja na Alli Kinduli mwamuzi msaidizi namba mbili wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Alphonce Mwandembwa na kamishna wa mchezo huo anatoka Seychelles, Lewis Blaze Madeleine
Wakati huo Mjumbe wa kamati ya Utendaji ya TFF Ahmed Msafiri Mgoyi ameteuliwa kusimamia mchezo wa Kombe la Shirikisho kati ya Club Desportivo Costa Do Sol ya Msumbuji na Cape Town City ya Africa Kusini utakaochezwa Machi 7, 2018 Estadio Nacional Dol Zimpeto,Maputo
Naye Makamu wa Rais wa TFF Michael Wambura ameteuliwa kusimamia mchezo wa Ligi ya mabingwa Africa kati ya Zesco ya Zambia na Asec Mimosas ya Ivory Coast itakayochezwa Machi 7,2018 Uwanja wa Levy Mwanawasa uliopo Ndola.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: