Timu ya Yanga imefanya mazoezi kwenye Uwanja wa Uhuru leo Alhamisi, huku mshambuliaji wake, Obrey Chirwa akifunga penalti.
Yanga imefanya mazoezi hayo ikiwa ni maandalizi ya mechi dhidi ya Azam FC Jumamosi.
Kikosi hicho kilifanyanya mazoezi kwa kupokezana baada ya timu mbili za daraja la kwanza kuutumia uwanja huo majira ya asubuhi
Katika mazoezi hayo ambayo yaliambatana na upigaji penalti, Chirwa alifanikiwa kufunga penalti yake baada ya kumuuza kipa Beno Kakolanya.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: